logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond amsifia Zuchu kwa kufikisha views milioni 100 kwa wimbo mmoja jukwaani YouTube

Wimbo wa Sukari ndio wa kwanza wa kiswahili usio na kolabo kufikisha views milioni 100.

image
na Davis Ojiambo

Burudani25 March 2024 - 06:35

Muhtasari


  • • Kando na rekodi hiyo, Zuchu pia ni mionhoni mwa wasanii wa kike katika ukanda wa Sub Sahara mwenye wafuasi wengi Zaidi katika mtandao wa video wa YouTube.

Bosi wa lebo ya muziki ya Diamond Platnumz, WCB Wasafi amevunja kimya chake na kudhihirisha furaha baada ya msanii wake Zuchu kuweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa kike Afrika Mashariki kufikisha utazamaji wa milioni 100 kwenye wimbo mmoja.

Zuchu ambaye alisainiwa kwenye lebo hiyo mapema 2020 na wikendi iliyopita alifikisha views milioni 100 kwenye wimbo wake wa Sukari, ambao aliuachia miezi michache baada ya kusainiwa.

Kufuatia ufanisi huo, bosi wake ambaye pia anatajwa kuwa mpenzi wake hakuweza kuficha furaha yake na kumuonea fahari Zuchu akisema kwamba mrembo huyo wa Zanzibar ameipa heshima lebo ya WCB.

Diamond alisema kwamba Zuchu ameiheshimisha lebo yake kwani wimbo wa ‘Sukari’ ndio wa kwanza wa Kiswahili usio wa kolabo kufikisha views milioni 100 kutoka kwa msanii wa kike.

Ukiona kwa macho ni kama Jambo la kawaida, ila sasa unapojaribu kufanya ndio unajua uzito wake!! SUKARI By female artist 100% Swahili song! No feature! 100M viewers! Ni heshima kwa WCB wasafi, music industry na nchi," Diamond aliandika kupitia kwa insta story yake.

Kando na rekodi hiyo, Zuchu pia ni mionhoni mwa wasanii wa kike katika ukanda wa Sub Sahara mwenye wafuasi wengi Zaidi katika mtandao wa video wa YouTube.

Wimbo wa ‘Sukari’ umetajwa na wengi kuwa bora kuwahi kutoka kwa msanii Zuchu, ambaye baadhi wanahisi ameshindwa kuishi kwa matarajio ya wengi ambao wanasema vibao vingine ambavyo amekuwa akichilia havijawahi piku kiwango cha ‘Sukari’.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved