Wikendi iliyopita, mchekeshaji Elsa Majimbo mwenye makao yake nchini Marekani aliwaunganisha wanamitandao katika mtandao mpya wa Threads baada ya kupakia video akivua nguo.
Majimbo hata hivyo alirudi baadae ba kukiri kwamba video hiyo hakuipakia kwa makusudi bali ilikuwa kimakosa, na akafafanua kuwa ilikuwa inakusudiwa kwenda kwa mpenzi wake na wala si kwa mashabiki wake mtandaoni.
Alirudi katika mtandao wa X na kuomba radhi kwa mashabiki wake huku akiwataka wote walioiona kuifuta kutoka katika fikira zao na kujifanya kama hawakuiona.
Alithibitisha kwamba Video hiyo ilikuwa mtandaoni kwa saa 18 kabla ya kuitambua.
Alifuta video hiyo ambayo ilizua gumzo kwa watumiaji wa mtandao. Majimbo aliomba msamaha wa dhati akitoa majibu kwa mashabiki waliohoji kuhusu video hiyo. Aliwataka wasahau kile walichokiona na wafanye kana kwamba hawakuona chochote.
“Kama kuna mtu ameona hiyo video chafu samahani sana. Hiyo ilikusudiwa mtu wangu. Sio mitandao ya kijamii, sahau na ufanye kana kwamba haujaona chochote! Najisikia vibaya sana kwa kufichua maudhui yasiyostahili kwenye umati wangu. Samahani kwa video hiyo guys makosa ya uaminifu, love y'all," alibainisha.
Majimbo akimjibu shabiki aitwaye Raymond aliyeuliza kilichotokea alisema;
"Baada ya kuangalia mavazi yangu jana nilifanya video nikivua nguo na kumtumia mpenzi wangu kisha kuiweka kwenye threads badala ya kuangalia mavazi yangu"
Aliwathibitishia mashabiki wake kwamba alikuwa amefuta video hiyo ya kusisimua na haikupatikana tena kwenye kalenda yake ya matukio kwenye nyuzi.
"Iko kwenye takataka ... Ilikuwa kwenye nyuzi kwa saa 18 kabla sijaona"