Jackie Matubia asherehekea hatua kubwa katika taaluma yake

Matubia ametangaza kukamilika kwa mradi mpya, akipeleka taaluma yake katika kiwango kingine.

Muhtasari
  • Alisimulia kuwa kufanya kazi kwenye mradi huo haikuwa rahisi, akibainisha amepigana vita vingi katika mchakato huo na amekuwa akiitwa majina.
MUIGIZAJI
JACKIE MATUBIA// MUIGIZAJI
Image: FACEBOOK//JACKIE MATUBIA

Muigizaji Jackie Matubia ametangaza kukamilika kwa mradi mpya, akipeleka taaluma yake katika kiwango kingine.

Mama huyo wa watoto wawili alishiriki habari njema kwamba kipindi cha youtube ambacho amekuwa akifanyia kazi kiko tayari na kitaonyeshwa kwa mara ya kwanza kwenye chaneli yake ya youtube mnamo Aprili 17, 2024.

Mfululizo unaoitwa "Toxic" utaleta hali ya maisha ya kila siku katika harakati kuu za mafanikio.

Matubia ambaye hivi majuzi alirejea nchini kutoka safari ya Malysia alisema kwamba alikuwa akihudhuria mikutano kadhaa kuhusiana na mradi ambao amekuwa akiufanyia kazi.

"Nimerudi tu nyumbani na kile nimekuwa nikifanyia kazi hatimaye kimekwisha. Nimeona picha na nimesikitika kihisia kwa kilio changu kibaya", mwigizaji alishiriki.

Wakati fulani Jackie alitokwa na machozi alipokuwa akiwahimiza mashabiki wake kutimiza ndoto zao, akibainisha kuwa wakati fulani, Ni watu wa karibu ambao hufanya kazi dhidi ya mafanikio ya mtu binafsi.

Alisimulia kuwa kufanya kazi kwenye mradi huo haikuwa rahisi, akibainisha kuwa amepigana vita vingi katika mchakato huo na amekuwa akiitwa majina.

"Acha nikuambie sio lazima iwe na maana kwa mtu yeyote. Ni lazima tu iwe na maana kwako. Na ikiwa ina maana kwako na Mungu anaendelea kukusukuma kufanya hivyo......Mungu nimefurahi sana. Kwa hivyo njoo, njoo huku nikiwaonyesha ninyi watu kile nimekuwa nikifanyia kazi na hatimaye umefika na wakati wa kushiriki nanyi".

"Nimewekeza kila kitu nilichopata kwa mradi huu na namshukuru Mungu nimefanikiwa. Nimepigana vita vingi sana, nimeitwa majina mengi sana!!! lakini niliamini neno la Mungu .... Atatengeneza meza. mbele ya adui zako.Siku moja nitasimulia hadithi yangu", Matubia alimalizia.