DJ Joe Mfalme, mapema Jumatatu alifajiri alifikishwa katika Mahakama ya Kibra kuhusu mauaji ya Inspekta wa Polisi kufuatia mzozo Machi 16.
DJ huyo alifika mahakamani pamoja na wafanyakazi watatu wake na maafisa watatu wa polisi walioshtumiwa kwa mauaji hayo.
Polisi waliomba kuwashikilia washukiwa hao kwa siku ishirini na moja zaidi ili kukamilisha uchunguzi kuhusu kisa hicho.
Maafisa watatu wa polisi waliohusishwa na kesi hiyo walikamatwa kwa mauaji ya mpelelezi wa Dagoretti anayehusishwa na Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) baada ya kuripotiwa kuingilia kati ugomvi wa tukio la trafiki lililohusisha DJ Mfalme na afisa huyo aliyefariki Machi 16.
Hizi hapa ni baadhi ya picha jinsi washukiwa hao walipandishwa kizimbani;