Amina Abdi amtetea Dj. Joe Mfalme baada ya tuhuma za mauaji

Ripoti zinaonyesha kuwa kama Dj. Joe Mfalme alikuwa akiondoka kwenye klabu mwendo wa saa 4:20 asubuhi, na makabiliano yakazuka

Muhtasari
  • Baadaye, Inasemekana vijana wa Joe Mfalme ilimtoa afisa huyo kutoka kwenye gari lake na kumpiga mateke na makofi kadhaa kabla ya kuondoka eneo la tukio.
Amina Abdi na Joe Mfalme
Image: Instagram

Mtangazaji wa TV Amina Abdi Rabar amejitokeza kumuunga mkono Dj. Joe Mfalme kufuatia kukamatwa kwake kuhusiana na kifo cha afisa wa DCI.

Katika video ya TikTok, Amina alisifu tabia za Joe akimtaja kuwa mtu mwenye bidii na mwenye huruma, na kusema kwamba DJ huyo ni mnyenyekevu na hawezi kumdhuru mtu yeyote.

"Joe Mfalme hana hatia, nimesema nilichosema, ni mtu mkarimu sana. Hawezi kumdhuru mtu. Hata wajaribuje kuipeperusha kwenye vyombo vya habari, watu wanaokujua wanajua HUWEZI KAMWE kufanya hivi. Mungu atakupitisha katika hili. Hili pia litapita ndugu yangu. Najua si wewe uliyefanya hivi. Hebu tuthibitishe kuwa hauna hatia", aliandika.

Dj Joe mfalme alijikuta  katika mikono ya kisheria mnamo Machi 24 baada ya kuhusishwa na tukio lililosababisha kifo cha afisa huyo.

Ripoti zinaonyesha kuwa Dj. Joe Mfalme alikuwa akiondoka kwenye klabu mwendo wa saa 4:20 asubuhi, na makabiliano yakatokea kati ya vijana wake na afisa wa DCI.

Inadaiwa kuwa, afisa huyo alikwaruza gari la DJ huyo, hivyo kuzua ugomvi mkali.

Baadaye, Inasemekana kuwa watu waliokuwa na Joe Mfalme walimtoa afisa huyo kutoka kwenye gari lake na kumpiga mateke na makofi kadhaa kabla ya kuondoka eneo la tukio.

Hali mbaya ya kiafya ya Kitosi ilisababisha kuhamishiwa katika Hospitali ya Lang’ata na baadaye Nairobi west Hospital, ambako aliaga dunia siku ya Alhamisi.

Licha ya uzito wa shutuma zinazomkabili Joe Mfalme, Amina Abdi bado yuko thabiti katika kumuunga mkono, akirejea hisia za wengine wanaothibitisha tabia na uadilifu wake.