Mboya atakuwa mfano kwa wengine:Shakila aapa kumshitaki Vincent Mboya

Shakila aliwaalika wanaume kujitetea akibainisha kuwa hakukusudia kukaa peke yake kwa muda mrefu.

Muhtasari
  • Baadaye Mboya alitoa matamshi kuhusu maisha ya kibinafsi ya Shakila (body count), ambayo yalimkasirisha sosholaiti huyo, na kumfanya kutishia kuchukua hatua za kisheria.
Vincent Mboya na Shakila
Image: Instagram

Shakila alirejea nchini na kukumbana na mambo ambayo hakuyatarajia hali iliyopelekea akabiliane vikali na mkuza maudhui Vincent Mboya.

Sosholaiti huyo wa Kenya, ambaye alikuwa akiishi Afrika Kusini kwa miezi kadhaa, alirejea nyumbani baada ya kuachana na mpenzi wake wa  raia wa Afrika Kusini.

Shakila alisema yuko tayari kupokea maombi ya wanaume wanaotaka kumchumbia akisema kwamba hakusudii kukaa peke yake kwa muda mrefu.

"Mimi niko single sasa. Tafadhali, hakuna mtu anayepaswa kudai kuwa yuko nami. Dm zangu ziko wazi", alichapisha kwenye Instastories yake.

"Hakuna wakati wa uponyaji. Chukua ndege inayofuata na uende kuwa na mwanamume anayestahili," sosholaiti huyo aliongeza.

Vincent Mboya alichukua fursa hiyo kujitetea kwa Shakila.

"Mpenzi Shakila naona uko single guess nani yuko single pia? Mimi ni kijana tajiri na maarufu. Tafadhali nijulishe mahali ulipo ninakuja kwa ajili yako. Kwa sasa ninasafiri kwa ndege kutoka Kanada kwa ajili ya mikutano fulani ya kibiashara lakini ninaweza kupita mahali ulipo nitakapomaliza, tayari kukuchunga vizuri", Vincent Mboya aliandika katika Instastories zake.

Baadaye Mboya alitoa matamshi kuhusu maisha ya kibinafsi ya Shakila, ambayo yalimkasirisha sosholaiti huyo, na kumfanya kutishia kuchukua hatua za kisheria.

“Hiyo kesi ya kashfa itakapokukuta, usiambie mashabiki wako wakuchangie pesa.......Mboya atakuwa mfano kwa wengine, huwezi kuweka midomo ya uvundo kwenye biashara ya kila mtu ili kufufua  kazi yako iliyokufa", Shakila aliandika.

Vincent Mboya hata hivyo hakushtushwa na tishio la Shakila kumshtaki akiapa kuendelea kumtafuta mwanamke ambaye atampenda.

"Niko single tena!! Sitaacha kujaribu bahati yangu na wanawake ambao wako single hadi siku nitakapompata anayefaa kabisa! Aluta Continua", Mboya aliandika.