Felicity Shiru, mpenzi wa YouTuber Thee Pluto ameonyesha nia ya kuwa tajiri kuitwa mama tena, miaka miwili baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza.
Shiru kupitia Instagram yake, alipakia video akiwa anacheza kwa kumpakata bintiye Zoey wakicheza na kuandika kwamba anahisi kuwa na utayarifu wa kutosha kujikita katika safari nyingine ya kuleta kiumbe kipya duniani.
Alisema kwamba katika siku za hivi karibuni, pindi anapomuona bintiye akicheza, anahisi kama ovary zake zinamtekenya, na kukisia kwamba hiyo inaweza kuwa ni ishara kutoka kwa mwili wake kuwa tayari kwa mimba nyingine.
“Mbona ovary zangu zinanitekenya? Mtoto nambari mbili pengine?” Felicity Shiru aliuliza huku akimtag baba bintiye Thee Pluto.
Katika chapisho hilo, Thee Pluto alimjibu akisema kwamba swali alilouliza kwa asilimia kubwa ndilo jibu.
YouTuber huyo mdogo mwenye utajiri mkubwa alionekana kuafikiana na pendekezo la mama bintiye kwamba ni wakati wa kutafuta mtoto mwingine na kuitanua familia hata Zaidi.
“Wasichana wangu. Hakina, namba 2 ni mpango tayari,” Thee Pluto alijibu.
Wawili hao wamekuwa pamoja kwa Zaidi ya miaka 3 na Pluto hivi majuzi alimjibu shabiki mmoja aliyeibua wasiwasi kwamba huenda mambo hayako sawa katika penzi lao.
Shabiki huyo alimwandikia ujumbe Thee Pluto na kumuuliza mbona hakumpost Felicity Shiru siku ya wapendanao ya Valentino, na kutaka kujua tatizo lilikuwa wapi hakuweza kupakia picha yake na kumwandikia ujumbe wa kimapenzi kama wafanyavyo wengine wengi katika mapenzi.
Hata hivyo, Pluto alijibu kwamba kila kitu kiko sawa na wala malalamiko kama hayo hayakutoka kwa Shiru bali kwa watu mitandaoni.