Mtangazaji Mwalimu Rachel ajiunga na Radio Africa Group

Radio Africa Group kwa sasa inamiliki Classic105, Kiss100, Radio Jambo, Homeboyz, Gukena, na East FM.

Muhtasari

•Bw Khafafa alisema Mwalimu Rachel ni mtangazaji mashuhuri na mwenye kipaji kikubwa na kwamba anafurahi amejiunga na kampuni ya Radio Africa Group.

•Mwalimu Rachael ni mtu maarufu na amekuwa akifanya kazi katika NRG kwa miaka 6 na amejenga kundi kubwa la mashabiki waaminifu.

GCOO wa Radio Africa Martin Khafafa akisalimiana na Mwalimu Rachel
GCOO wa Radio Africa Martin Khafafa akisalimiana na Mwalimu Rachel
Image: BRIAN SIMIYU

Mtangazaji Mwalimu Rachel amejiunga na kampuni ya Radio Africa Group.

Katika tangazo lililotolewa na Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Kundi, Martin Khafafa alisema kwamba mtangazaji huyo maarufu wa redio amekubali nafasi katika jumba hilo la wanahabari lenye makao yake makuu Westlands.

Alimwambia Kalondu Musyimi wa Mpasho kwamba Mwalimu Rachel ni mtangazaji mashuhuri na mwenye kipaji kikubwa na kwamba anafurahi amejiunga na kampuni ya Radio Africa Group.

"Tunafuraha kwa fursa tutakayompa ili ajiunge na Radio Africa Group ambayo ni nyumbani kwa vipaji bora vya redio nchini."

Aliongeza,

"Tutampa sapoti ya hali ya juu na ni wazi wasikilizaji kwenye mitandao ya kijamii wanafurahishwa sana na matarajio ya kujiunga kwake. Tunatazamia kuwahudumia wasikilizaji wetu na watangazaji kwa ununuzi mwingine mkubwa katika Radio Afrika."

Na atajiunga na kituo gani?  "Nitamuachia hilo msimamizi wa programu," alielezea.

Kwa nini kampuni ya habari ilimchagua Mwalimu Rachel?

 Bwana Khafafa alikuwa na jibu la kina ambapo alisifu fadhila za kampuni na Rachel.

“Ni wazi kwamba kila mtangazaji chipukizi anataka kujiunga na Radio Africa, na kwangu mimi ni kumpa mtu nafasi kadri tunavyohisi kuna nafasi ya kustawi.

Nadhani Radio Africa imetoa talanta kubwa mtandaoni kutoka kwa Maina Kageni, Mwalimu King'ang'i. Kwa hivyo watu wanatambua kuwa Radio Afrika ndio mahali pa kutambua uwezo wao wa anga na vipaji vyao."

Radio Africa Group kwa sasa inamiliki Classic105, Kiss100, Radio Jambo, Homeboyz, Gukena, na East FM.

Mwalimu Rachael ni mtu maarufu na amekuwa akifanya kazi katika NRG kwa miaka 6 na amejenga kundi kubwa la mashabiki waaminifu.

Yeye pia ni mtangazaji wa hafla, meneja wa talanta, mzungumzaji wa motisha, msanii wa sauti, na mjasiriamali.