•Kulingana na maelezo kwenye picha hiyo, marehemu Brian Chira alimpoteza mama yake mnamo Agosti 15, 2008.
•Marehemu Brian Chira alikuwa na umri wa takriban miaka minane tu wakati alipofiwa na mama yake.
Picha ya zamani ya marehemu Brian Chira wakati wa mazishi ya mama yake miaka mingi iliyopita imegusa watumiaji wengi wa mtandao.
Picha hiyo iliyopigwa takriban miaka kumi na sita iliyopita iliibuka Jumanne, Machi 26, siku ambayo marehemu Chira alikuwa akizikwa katika eneo la Githunguri Kiambu.
Kulingana na maelezo kwenye picha hiyo, marehemu alimpoteza mama yake mnamo Agosti 15, 2008. Bi Sophia Wambui alikuwa na umri wa miaka 28 tu wakati alipofariki, kwani alikuwa amezaliwa Julai 20, 1980.
Marehemu Brian Chira alikuwa na umri wa takriban miaka minane tu wakati alipofiwa na mamake, na akaachwa mikononi mwa nyanyake, Esther Njeri.
Wanamitandao wameendelea kutoa hisia mseto kuhusu picha hiyo baadhi wakionekana kumhurumia marehemu Chira, wengine wakipongeza jinsi alivyokuwa mjasiri, na wengine hata wakibaini maelezo kuhusu jinsi mama yake alivyokuwa mdogo alipofariki mwaka wa 2008.
Kundi la watumiaji wa mtandao wamelinganisha kifo cha mwanatiktok huyo na kile cha mama yake kwani wote wawili walikufa wakiwa na umri mdogo sana.
Tazama maoni ya baadhi ya wanamitandao;-
Peris_Wambuthia: Seems his mum died at a younger age as well.
Basic_posh: God please keep us to raise our children until they are grown.
Jaluomoja: People don’t realize how much traumatic damage a child undergoes emotionally when they loose loved ones, especially their mom at an early age! He endured a lot of hardships.
Christinewallei: Kids suffer when parents die.
Wambuijoseph11: This boy really suffered, I can’t imagine being an orphan at that age.. I wish people did something to help when he was still alive. Just a wish. May God keep our parents us who are parents for long enough to see our kids grow and prosper.. Rest in peace Chira.
Mamia ya Wakenya Jumanne walijitokeza kwa mazishi ya marehemu Brian Chira nyumbani kwa familia yake Gathanje, kijiji cha Ingitei, Githunguri katika Kaunti ya Kiambu.
Siku ilianza kwa kutazamwa na kukusanywa kwa miili katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Msafara wa magari yaliyokuwa yakielekea kwenye mazishi ya Tiktoker huyo yalionekana yakisimama katika Hospitali kwa ajili ya kutazama miili.
Waombolezaji walifuata msafara hadi eneo la maziko yake katika kaunti ya Kiambu.
Ulikuwa ni wakati wa hisia kwa waombolezaji huku wakiutazama mwili wake ukishushwa kaburini.