logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Simon Kabu kuwapeleka Baba Talisha na nyanyake Brian Chira likizo ya siku 3 na usiku 2 Diani

Baba Talisha na nyanyake Brian Chira walisimama kidete na kuona michango ikifika hadi milioni 8.

image
na Davis Ojiambo

Burudani27 March 2024 - 13:38

Muhtasari


  • • Awali, wanamitandao walimuomba Baba Talisha kuendelea kumshika mkono nyanya huyo baada ya kusimama naye katika kipindi cha wiki mbali tangia mjukuu wake alipofariki.
Baba Talisha na nyanyake Chira.

Afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya kusafirisha watalii ya Bonfire Adventures, Simon Kabu ameonesha kuguswa na jinsi tiktoker Baba Talisha alivyojifunga kibwebwe na kuwa kwenye mstari wa mbele kuongoza na kufanikisha mazishi ya Brian Chira.

Kabu kupitia ukurasa wake wa Instagram, alisema kwamba kutokana na kuguswa huko, kampuni yake ya Bonfire Adventures imeamua kumtunuku Baba Talisha na nyanyake Chira likiza ya siku tatu na usiku 2 kujivinjari katika fukwe za Diani kaunti ya Kwale.

Kabu alisema kwamba ni wawili hao sasa kukubali na kuchagua siku ambazo watakuwa wanataka kwenda kutumikia likizo yao ya kujivinjari Diani.

“Baba Talisha … na Shosho ya Chira. Nadhani baadhi ya juhudi zinastahili kutambuliwa. BONFIRE ADVENTURES imewalipia siku 3 usiku 2 Likizo ya kwa nijia ya ndege kwenda Diani kwa wakati muupendao,” alisema.

Baba Talisha na nyanyake Brian Chira walisimama kidete na kuona michango ikifika hadi milioni 8 mitandaoni iliyokusudiwa kuendesha shughuli zote za mazishi na zingine zisalie kumsaidia mkongwe huyo.

Awali, wanamitandao walimuomba Baba Talisha kuendelea kumshika mkono nyanya huyo baada ya kusimama naye katika kipindi cha wiki mbali tangia mjukuu wake alipofariki.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved