Mwanamume mmoja kutoka sehemu za Magharibi mwa Kenya amechukua kwenye mtandao wa TikTok akiweka msururu wa picha zake kwenye muundo wa video bango la kumtongoza tiktoker Nyako Pilot.
Kijana huyo kwa jina Ainea Nabwera alionekana akiwa ameshikilia bango lenye ujumbe uliokusudiwa kumfikia TikToker huyo ambaye anaishi Ujerumani.
Nabweri katika ujumbe wake wa kumtupia ndoana ya mapenzi Nyako, alimhakikisha kwamba pindi atakapompenda basi ajue kwamba hajafanya uamuzi mbaya kwani hakuna siku atawahi lala njaa wakiwa wapenzi.
Nabweri alisema kwamba kwa kumhakikishia hilo, mwanzo Nyako ajue kwamba yeye ni mmiliki wa mashine ya kusiaga mahindi na kutengeneza nafaka kwa lugha ya mtaani ‘kisiagi’ jambo ambalo litahakikisha unga unapatikana kwake muda wote saa ishirini na nne kwa wiki.
“Nyako ninataka kukuoa, mimi ni Mluhya ninamiliki posho-mill hivyo hautalala njaa,” sehemu ya ujumbe kwenye bango lake ulisoma.
Hata hivyo, mpaka wakati taarifa hii ilikuwa inachapishwa, Nyako hakuwa ametoa jibu kwa kijana huyo lakini baadhi ya watumizi wa TikTok walikuwa na haya ya kusema;
“Nyako akijibu niitwe ndio nijuwe kma ndacommet ama hapana 😂😂 anyway all the best braza,” Nzish Mkisa.
“Wacha Nyako aone hii, comeback utapata utatii kaka,” Mama Leon2019.
“Wewe unajitafutia shinda tena kwa bei nafuu kabisa,” Prossy.
Katika video hiyo, kijana huyo aliiambatanisha na wimbo wa ‘Salima’ wake Linex Sunday aliomshirikisha Diamond Platnumz mwaka 2015.