Baba Talisha, tiktoker aliyesimamia miamala yote ya michango kwa ajili ya kufanikisha hafla ya mazishi ya tiktoker mwenza, Brian Chira hatimaye ametoa maelezo jinsi michango hiyo iliyotumika.
Baba Talisha ambaye mpaka siku ya mazishi aliwataarifu mashabiki wake kwamba michango ilikuwa imevuka shilingi za Kenya milioni 8 alikwenda live kwenye tiktok na kuwaalika wenzake ambao walishirikiana katika kufanikisha mchango huo mkubwa.
Baba T kando na kuwaalika wenzake kwenye live, aliwatumia pia nyaraka za maelezo ya jinsi michango yote kupitia M-Pesa na benki ilivyoratibiwa na kutumiwa, lakini pia kiasi cha pesa zilizosalia na kazi yake ya baadae baada ya Chira kuzikwa wiki jana.
Baba Talisha alieleza ni hela ngapi kutokana na michango hiyo ambazo zilitumika katika usafiri kutoka Nairobi kwenda Githunguri kwa nyanyake Chira alikozikwa, vyakula, maturubai miongoni mwa vitu vingine.
"KSh 498, 125. Ilitubidi kununua vyakula vingine. Hapo awali tulipanga bajeti ya watu 600 au 700, lakini wakati wa mazishi, tulilazimika kuongeza chakula zaidi. Tulilipa amana ya 105,000, na tulikuwa na nakisi ya 29,000, na tulilipa yote," Baba Talisha alianza kudadavua mahesabu.
Baba T pia alifichua kuwa kiasi kilichosalia ni KSh 7.2 milioni baada ya kulipa walichokuwa wakidaiwa. “Balance iko kwa benki ni KSh 7.2 milioni. Baada ya nimemaliza kulipa deni, nyanyake Chira amepewa taarifa kwamba kwa mwezi wa tano, anafaa kuwa kuhama huko, hivyo tunatakiwa tuwe na haraka,” Baba T alisema.
Tazama video hii jinsi alidadavua hesabu zote;