Ulinipa nafasi katika umri wangu kuwa mke- Esther Musila amsifia mumewe Guardian Angel

Akizungumzia jukumu lake katika maisha ya mumewe, alimshukuru kwa kumchagua, na bila kujuta.

Muhtasari

•Wanandoa hao walihimiza familia na zaidi wazazi na washauri wa mitandao ya kijamii kuwa wazi kuhusu hali kama hizo.

•"Inatoka ndani yangu kwa kawaida kuwa tu mke, na hii inatokana na jinsi unavyonitendea, heshima unayonipa, urafiki tulio nao," alisema Bi Musila.

Esther Musila na mumewe Guardian Angel
Image: INSTAGRAM// ESTHER MUSILA

Ndoa kati ya Esther Musila na mwimbaji wa nyimbo za Injili Guardian Angel inaendelea kuvuta maoni kutoka kwa jamii miaka minne hadi sasa.

Maoni juu yao ni kitu ambacho wamekua wakipuuza haswa mitandao ya kijamii.

Wanandoa hao walizungumza kwenye chaneli yake ya YouTube ambapo alihimiza familia na zaidi wazazi na washauri wa mitandao ya kijamii kuwa wazi kuhusu hali kama hizo. Walisema Mungu amekuwa mwaminifu kwa ndoa yao.

"Niko mahali katika maisha yangu ambapo sasa ninaelewa nini hasa kuolewa kunahusu," akisema amejifunza kuwa na nidhamu na kuwajibika.

Walizungumza kuhusu ukuzi na mambo waliyopitiakama wanandoa.

 Akizungumzia jukumu lake katika maisha ya mumewe, alimshukuru kwa kumchagua, na bila kujuta.

"Umenipa nafasi katika umri wangu wa kuwa mke. Watu wanapotaja mahusiano kuwa mke, majukumu ambayo unayafanya katika maisha ya mumeo, haya kwangu yanaibua ukweli, kana kwamba mimi ni mke. .

Inatoka ndani yangu kwa kawaida kuwa tu mke, na hii inatokana na jinsi unavyonitendea, heshima unayonipa, urafiki tulio nao."

Wana pengo kubwa la umri. Esther aliongeza,

"Mimi kuwa mkubwa kiumri kuliko wewe haijawahi kunifanya nijisikie kuwa nina mamlaka ya aina yoyote. Wewe ndiye kichwa cha familia, kwa hiyo watu wengi watafikiri kwamba oh kwa sababu Esther ni mkubwa ndiye anayeweza kusema. Unajua?.. .Hapana," akatikisa kichwa.

Guardian alizungumzia dhana hii potofu, “Kama mtu lazima awe na mamlaka haihusiani na umri, mtu akiwa na mke mwenye kichwa ngumu, kichwa nguu hakihusiani na umri."