Mwimbaji Mshindi wa Tuzo wa Nigeria Wizkid amekuwa gumzo mitandaoni baada ya kumtupia jibu la kijeuri mtumizi mmoja wa X aliyekataa kukubaliana na kauli yake.
Wizkid kupitia X aliandika kauli fupi kwamba Pesa haziweni nunua upendo lakini mtumizi mmoja akwa wa haraka kumjibu kwamba hawezi katu kukubaliana na kauli hiyo.
Hata hivyo, Wizkid hakuweza kuimeza kauli hiyo ya kukanusha kauli yake na alimpiga kumbo kali shabiki huyo, akimshambulia kwa kigezo cha mzazi wake.
Kupitia ukurasa wake wa X uliothibitishwa, Wizkid alipokuwa akizungumza kutokana na uzoefu alisema kuwa pesa haiwezi kununua mapenzi ya dhati.
Wizkid aliandika; "Pesa hainunui Upendo."
Akijibu, shabiki anayejulikana kama Beela1 alikataa kukubaliana na Wizkid kufichua kuwa pesa inatosha kununua mapenzi.
Beela1 aliandika; "Bosi sikubaliani."
Jibu hili halikukaa vyema kwa Mshindi wa Tuzo ya Grammy kwani alijibu kwa kushambulia sura ya baba ya shabiki.
Wizkid aliandika; "Hiyo ni biashara ya baba yako."
Jibu hili la Wizkid lilizua hisia tofauti mtandaoni, huku baadhi wakisimama naye, wengine wakimkabili mwimbaji huyo kwa kumshambulia mzazi wa shabiki huyo kwa kumjibu kwa shari.
stardomset: ππππ Yeah huyo Wizkid twitter vibe amerudi π₯ mshenzi.
rxea_boy: Wiz mkubwa mwenye mdomo mbaya kila mara kwenye ushenzi π.
@DanielRegha: Wizkid kumhusisha baba wa mtu katika kujibizana au kujibu ni kukosa heshima; Mashabiki wanashangilia sasa lakini Burna alikuwa amesema yaleyale "That one na ur papa business". Unafiki unaugua.