logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Otile Brown atangaza kuachilia wimbo wake wa injili wiki chache baada ya kuachia albamu

Ujio wa wimbo huo unakuja wiki chache baada ya kuachia albamu yake yenye ngoma 15.

image
na Davis Ojiambo

Burudani04 April 2024 - 09:04

Muhtasari


  • •  Katika wimbo huo kwa sehemu, msanii huyo anasikika akiguguna maneno kwamba hata kwenye ajali wala kifo haogopi wakati anajua kwamba Mungu wake yuko karibu naye kila wakati.
  • • Ujio wa wimbo huo unakuja wiki chache baada ya kuachia albamu yake yenye ngoma 15.
OTILE BROWN

Siku chache baada ya kufokewa vikali na mashabiki katika tamasha la Raha Fest, msanii Otile Brown ametangaza kuachilia wimbo wake wa kwanza wa injili.

Kupitia Instagram yake, Otile Brown alipakia klipu aliimba wmbo huo na kuandika kwamba ni wimbo wake wa kwanza wa injili na ambao utatoka Kesho Ijumaa ya Aprili 5.

Akizungumza kuhusu himizo nyuma ya utunzi wa huo wimbo kwa jina ‘Hafanani’, Otile alisema kwamba ameimba juu ya vitu vingi lakini safari hii angependa kuimba juu ya Mungu.

“#Hafanani inashuka kesho... wimbo wa kwanza wa injili. Ngoja nimwimbie Bwana, niliimba mambo mengi lakini sikumwimbia kamwe 😔 mshuhudie kwa sauti yangu kesho,” Otile Brown alisema.

 Katika wimbo huo kwa sehemu, msanii huyo anasikika akiguguna maneno kwamba hata kwenye ajali wala kifo haogopi wakati anajua kwamba Mungu wake yuko karibu naye kila wakati.

Haya hapa ni baadhi ya maneno kwenye mishororo yake;

“Nimeshindikana, tena siogopi hata kwa ajali, ilmradi uko nami, niko sambamba, siogopi hata kwa ajali maana Mungu wangu mimi hafanani, yeye hafanani na binadamu…”

Ujio wa wimbo huo unakuja wiki chache baada ya kuachia albamu yake yenye ngoma 15 ikiwemo ‘One Call’ ambayo iliibuka kuwa pendwa kwa baadhi ya Wakenya haswa kutokana na kifo cha tiktoker Brian Chira.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved