logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Otile Brown avunja kimya kuhusu tukio la mashabiki kumfokea akiwa jukwaani Raha Fest

Otile alitumia fursa hiyo kutoa neno moja kwa wale anaodai walipanga njama ya kumdhalilisha.

image
na Davis Ojiambo

Burudani04 April 2024 - 14:24

Muhtasari


  • • Pia msanii huyo alifafanua kuhusu tukio lake kuonekana akiondoka jukwaani na kurudi baada ya sekunde kadhaa huku mashabiki wakizidi kufoka.
Otile Brown

Msanii wa kizazi kipya kwa mara ya kwanza amevunja kimya kuhusu klipu inayoenezwa mitandaoni ikimuonyesha akitupiwa maneno na mashabiki akiwa jukwaani wakati wa tamasha la Raha Fest wikendi iliyopita.

Akizungumza na mashabiki wake kwenye kipindi cha mubashara kupitia TikTok, Otile Brown alisema kwamba watu waliomfokea si mashabiki bali ni watu waliolipwa na baadhi ya mahasidi wake kimuziki ili kumdhaliisha.

Pia msanii huyo alifafanua kuhusu tukio lake kuonekana akiondoka jukwaani na kurudi baada ya sekunde kadhaa huku mashabiki wakizidi kufoka.

“Shoo ilikuwa vizuri tu, ni hapo mwanzo tu na ambapo waliichukua na kuikata ikawa vile, kwa sababu nilikuwa nimeambiwa nina dakika 7 za kutumbuiza. Walikuwa na intro yangu na wakati wanaicheza sikuisikia hivyo ikanichochea kurudi nyuma baada ya kugundua sina in-ears kwa sababu sikuwa najisikia,” Otile alifafanua.

“Kwa hiyo kilichotokea ilinibidi niende kuchukua in-ears zangu na watu walikuwa tayari wanafoka. Watu waliokuwa mbele walikuwa wanataka nisogee karibu nao, lakini waliokuwa wameletwa pale ili kunidhalilisha ni wachache, na lile tukio lilikuwa limepangwa kabisa,” Browm alizama Zaidi katika maelezo.

Otile alitumia fursa hiyo kutoa neno moja kwa wale anaodai walipanga njama ya kumdhalilisha kwa kuweka watu sehemu Fulani ili kumpigia kelele akitumbuiza.

Kwa maneno yake, alisema;

“Hao jamaa katika ng’ambo hiyo nyingine, mimi hamniwezi mzee. Sawa, mimi nataka mjue tu, hamniwezi na leo nasema. Na mnajua hiyo ndio maana mnaanza kuungana makundi makundi, kama unajiamini mbona usije twende sawa?”


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved