Akuku Danger afunguka jinsi mume wa 'mumama' wake alivyowafumania Kilimani

Alisimulia zaidi jinsi alivyopewa pesa baada ya kuingia kwenye gari la kifahari alilokuwa akimiliki mwanamke huyo.

Muhtasari
  • Alisimulia jinsi alivyokutana na mwanamke  baada ya shoo yake kwenye hafla na wakati huo, Akuku Danger alidai kuwa bado alikuwa chuo kikuu.
Akuku Danger
Image: Radiojambo

Mannerson Oduor anayejulikana pia kama Akuku Danger ameshiriki tukio la maisha ambalo lilikaribia kugharimu maisha yake.

Mchekeshaji huyo kupitia mahojiano, alifichua tukio hilo na mumama ambalo lilimfundisha somo la maisha.

Alianza kwa kusimulia jinsi alivyokutana na mwanamke  baada ya shoo yake kwenye hafla na wakati huo, Akuku Danger alidai kuwa bado alikuwa chuo kikuu.

"Kitambo nikiwa campus, nilikuwa napiga shughuli moja mbili pale. So siku moja after kupiga show yangu pale Carnivore nikaona mwana dada mmoja hivi akaniambia Kijana napenda show yako. Akaniambia niingie kwa gari anidrop. Wakati huo bado nilikuwa mtu wa mguu. Nikasema kwa nini isiwe hivyo? Nikaingia kwa gari teketeke," Akuku Danger alisema.

Mchekeshaji huyo aliamini baada ya kishawishi ambacho alipokea .

Alisimulia zaidi jinsi alivyopewa pesa baada ya kuingia kwenye gari la kifahari alilokuwa akimiliki bibi huyo.

“Alikuwa anaendesha Mercedez. Sikuwa najua kuna wamama Nairobi. Kidogo akaconfuse kijana, nikaona pesa sijawahi ona katika maisha yangu. Ukinagalia paja yake pia ni ya thao. Akaniuliza pahali nasomea nikamwambia".

“Akaniambia nichukue 20,000K nikaingiza kwa mfuko. Kufika Lang’ata hapo kwa barabara nikangoja gari za rongai lakini magari zilikuwa zimejaa. Akaniambia tuwende kwake Kilimani kwa usiku alafu niende kwangu asubuhi,”alisema

Baadaye, mcheshi huyo alikubali kwenda naye nyumbani kwake. Kwa bahati mbaya, mume wa mwanamke huyo alijitokeza

Tukafika kwa nyumba. Aliniambia nijisikie huru nyumbani. Ikafika wakati wa kulala akuliza kama anaweza kuungana nami au ungependa kuungana naye? Alijiunga nami na kila kitu kilifanyika.

"Kidogo kidogo mtu akagonga mlango…"

Hivi ndivyo alivyoweza kutoka katika hali hiyo;

"Kabla tufungue akaniambia niave nguo alafu nijifanye nimelala.  Huyo jamaa akakuja kwa room nilikuwa akafungua stima. Nikatoa macho nje nikamsalimia nikamdanganya yeye ni rafiki yangu tu. Nakuambia ni Mungu tu alinitoa kwa  hali hiyo. Huyo jamaa alikasirika lakini aliona mi ni mdogo sana akaona hakuna kitu anaeza nifanyia,” Akuku Danger alieleza