Mtangazaji wa kipindi cha Bustani la Massawe kwenye Radio Jambo, Massawe Japanni amesherehekea hatua kubwa katika safari yake ya kupunguza uzito wa mwili.
Siku ya Alhamisi, mtangazaji huyo mahiri wa redio alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuwasasisha mashabiki wake kwamba tayari amepunguza kilo 10 za uzito wa mwili wake.
Pia alisherehekea kujenga misuli katika kipindi ambacho amekuwa akifanya mazoezi.
"Scream muscle ... 40 and Ciao.. Na ndio, nimetia bidii kwa mwili wangu," Massawe alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Malkia huyo wa redio aliambatanisha taarifa yake na picha nzuri inayoonyesha jinsi mwili wake ulivyo mzuri baada ya mabadiliko hayo.
"Kilo 10 zimepungua. Nasherehekea misuli niliyopata katika safari yangu," aliongeza.
Mama huyo wa mabinti watatu warembo amekuwa akienda kwenye chumba cha mazoezi na amekuwa akifanya mazoezi kwa bidii kwa muda sasa.
Massawe amekuwa akishiriki safari yake ya mazoezi na mashabiki wake kwenye majukwaa yake ya mitandao ya kijamii kupitia video na picha za kutia moyo.
Kweli, juhudi zake zinazaa matunda kwani hatua kwa hatua anapata matokeo aliyotaka.