logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mungu tu ajuaye! Staa wa Dancehall Buju Banton amuomboleza mwanawe wa miaka 20

Kakake alisema kuwa Miles alikuwa akiishi Marekani wakati wa kifo chake.

image
na Samuel Maina

Burudani05 April 2024 - 10:06

Muhtasari


  • •Miles ambaye alikuwa na umri wa miaka 20 wakati wa kifo chake alifariki nchini Marekani siku chache zilizopita.

Gwiji wa dancehall kutoka Jamaica Mark Myrie almaarufu Buju Banton na familia yake wanaomboleza kufuatia kifo cha mwanawe Miles Myries.

Miles ambaye alikuwa na umri wa miaka 20 wakati wa kifo chake alifariki nchini Marekani siku chache zilizopita.

Buju alithibitisha habari hizo za kuhuzunisha kwenye mtandao wa Instagram ambapo alishiriki picha ya maregemu mwanawe , na kuandika maneno " “Sip papa God knows.”

Kumaanisha: “Ni Mungu tu ajuaye.”

Hapo awali mnamo siku ya Jumatatu, Jahazeil Myrie, mwana mwingine wa Buju Banton, awali alikuwa amethibitisha habari hizo za kusikitisha kwa Observer Online.

"Ndio ni kweli. Sio jambo langu kusema, sio kazi yangu mwenyewe kutoa habari zozote za kibinafsi za Miles, baba yangu ndiye anayepaswa kutoa maelezo yoyote.

Lakini Miles ni kijana mzuri, roho yake ilikuwa safi, kwa hivyo nililazimika sema kitu." Jahazeil alisema.

Alisema kuwa Miles alikuwa akiishi Marekani wakati wa kifo chake.

Hata hivyo hakufichua sababu ya kifo au iwapo kaka yake alikuwa mgonjwa.

Msanii wa kundi la Morgan Heritage, Gramps Morgan alimuomboleza kijana huyo katika ujumbe akisema;

MIGHTY MY HEART IS WITH YOU BREDDA PRAYERS WITH YOU THE MOM AND FAMILY STAY ATRONG MI BREDDA!!" 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved