Mtayarishaji wa maudhui maarufu wa Kenya Kelvin Kinuthia ameweka mambo bayana kuhusu jinsia yake halisi.
Akizungumza kwenye mahojiano na Mungai Eve, Kinuthia aliwataka watu kujihusisha na mambo yao wenyewe, akisema kuwa mijadala kuhusu kundi la LGBTQ haina uhusiano wowote naye.
Kulingana na TikToker huyo, kila mtu ana haki ya kuishi maisha yake na kutambua anavyotaka.
Akijibu swali la moja kwa moja kuhusu uhusiano wake na kundi la LGBTQ, Kinuthia alishikilia kuwa maisha yake ya kibinafsi, ikiwa ni pamoja na jinsia na mapendeleo yake ya kimapenzi, yanasalia kuwa mambo yake ya kibinafsi.
Alisisitiza kuwa jinsia na upendeleo wake wa kuchumbiana ni biashara yake mwenyewe.
"Nilipata watu wakiuliza lakini hiyo ni swali mbaya.......kama uko ndani uko ndani.....hiyo ni stori yako mimi hainihusu," alisema.
"Kama niko, ni maisha yangu. Kama siko, ni maisha yangu pia," Kinuthia aliongezea.
Kinuthia pia aligusia usumbufu anaopata watu wanapomuita mwanaume, haswa akiwa amejipamba kikamilifu katika mavazi ya kike.
Ingawa alisema haoni jambo la kuudhi haswa, anapendelea zaidi wamwite kwa jina lake.
“Kuna wakati ulisema ukikutana na mashabiki wako wa kiume huko nje waache kukuita kaka, ulisema unajitambulisha kuwa ni mtoto wa kike...kwanini ukawa na hamu ya kuwaambia ‘mkue mnaniita Babygirl?" Eve aliuliza.
"Siwezi sema nimechukizwa inakaanga mbaya....fikiria umeng'ara uko katikati ya mall halafu mtu anawika, 'niaje bro'........Siezi sema huwa naipata mbaya, naona tu ikiwa shida" , Kinuthia alijibu.