Mtayarishaji wa maudhui na mwanzilishi wa Kenya Online Media, Director Trevor, amefunguka kuhusu hali yake ya uhusiano na mwanamke bora kwake.
Mjasiriamali huyo kijana alikanusha madai ya kuwa kwenye uhusiano na mtu yeyote wiki chache tu baada ya kuachana na ex wake, Mungai Eve.
Hivi majuzi Trevor alikuwa amewaacha Wakenya wakishangaa kama kwamba amepata mpenzi mpya baada ya kushiriki picha za mwanamke ambaye alifunika uso wake.
Hata hivyo, alithibitisha kwamba mwanamke huyo alikuwa rafiki yake tu na kuweka wazi kuwa bado yuko sokoni, kinyume na walivyofikiri wengi.
"Alikuwa rafiki tu, na tulikuwa nje. Sasa hivi, ningetaka mwanamke ambaye anafanya kazi. Anapaswa kuonekana jinsi anavyoonekana. Unajua muonekano sio muhimu sana, tunaweza kununua sura. Hayo mambo mengine anapaswa kuwa nayo kwa hivyo asijali. Anaweza kuwa mkubwakuniliko au mdogo kuniliko," alisema.
Pia alieleza sababu ya kutomtakia siku njema ya kuzaliwa mpenzi wake wa zamani Eve Mungai ambaye hivi majuzi alitimiza miaka 24.
“Kama ningetaka kumwish ningemwish kwenye DM yake binafsi lakini sio mtandaoni kwa sababu watu wa mtandaoni hawaelewi, wanasukuma tu vitu ambavyo havipo, nahisi ni wakati mwafaka wa kufocus kwenye mambo yangu na pia yeye nimpe nafasi ya kuzingatia mambo yake,” aliongeza.
Trevor pia alifichua mipango ambayo inamlazimu kumnunulia gari mtangazajiwake wa sasa, Eve Nyaga mnamo siku yake ya kuzaliwa.
"Siku yake ya kuzaliwa ni Aprili 23, lakini nataka hiyo iwe surprise, kwa hivyo tayari nimepata gari. Nitalifungua," alisema zaidi.