logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wahu ashindwa kuficha furaha yake bintiye wa miezi 17 akihesabu moja hadi kumi kwa ufasaha

“Haka ni kerevu kama mama yake,” Wahu alisema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani11 April 2024 - 06:43

Muhtasari


  • • Binti huyo aliyezaliwa mwezi Oktoba mwaka 2022 mpaka sasa ana miezi 17 lakini alionekana kuwa makini katika kuhesabu takwimu hizo ambazo aghalabu huwapa changamoto watoto wa umri wake.
WAHU

Familia ya Nameless na Wahu Kagwi wana furaha baada ya binti yao mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 5 kung’amua kukariri kwa kuhesabu nambari moja hadi 10.

Wahu alijionea fahari kwa kitinda mimba wake na kupakia video hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram, akimtaja binti huyo kama mtoto mwerevu kupindukia.

Hata hivyo, msanii huyo hakuweza pia kujitapa akisema kuwa bla shaka werevu wa bintiye ni kama wa mama yake.

“Haka ni kerevu kama mama yake,” Wahu alisema.

Binti huyo aliyezaliwa mwezi Oktoba mwaka 2022 mpaka sasa ana miezi 17 lakini alionekana kuwa makini katika kuhesabu takwimu hizo ambazo aghalabu huwapa changamoto watoto wa umri wake.

Mashabiki wake walimpongeza kwa kazi kubwa katika malezi ya mtoto huyo.

Hizi hapa ni baadhi ya pongezi;

“Huyu mtoto amefikisha mwaka mmoja?...brilliant” mmoja aliuliza ambapo Wahu alijibu kwamba ana mwaka mmoja na miezi 5.

“Huyu atasoma jalada lote la katiba ya 2010 mwanzo hadi mwisho👏👏atakapofikisha miaka 3,” shabiki mwingine alisema.

“Mtaalamu wa hisabati, tunda halikuanguka mbali na wahu,” mwingine alisema.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved