logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Nitakuwa Mwafrika wa kwanza kutazama Arsenal ikicheza 'live' ¼ fainali ya UCL” – Alinur

Mtanange huo mkali utaamua nani atakayejiunga na Borrusia Dortmund na PSG kwenye nusu fainali.

image
na Davis Ojiambo

Burudani17 April 2024 - 10:35

Muhtasari


  • •  Akizungumza kama shabiki wa Arsenal, Alinur alisema kuwa ana matumaini ya Zaidi ya asilimia 100 kuwa timu yake itafuzu kuingia nusu fainali kwa kuichabanga mwenyeji Bayern Munich.
  •  
    •  Pia alisema kuwa ana mpango wa kuialika timu nzima ya Arsenal kuja Kenya ili kuwapa motisha vijana wapenda soka.
Alinur Mohamed.

Aliyekuwa mgombea wa ubunge Kamkunji, Alinur Mohamed ambaye ni shabiki kindakindaki wa Arsenal amefichua kwamba ameelekea nchini Ujerumani kushuhudia mubashara mtanange wa robo fainali ya ligi ya mabingwa baina ya Bayern Munich na Arsenal.

Mtanange huo mkali utaamua nani atakayejiunga na Borrusia Dortmund na PSG kwenye nusu fainali, ikiwa raundi ya kwanza mechi iliisha sare ya mabao 2-2 ugani Emirates nchini Uingereza.

Alinur alisema kwamba atakuwa Mkenya na Mwafrika wa kwanza kuwahi kushuhudia mechi ya moja kwa moja ya robo fainali ya ligi ya mabingwa inayohusisha timu ya Arsenal.

“Nimeondoka nchini kwenda kujiunga na Arsenal nchini Ujerumani katika uwanja wa Allianz Arena. Nitakuwa Mkenya wa kwanza na Mwafrika wa kwanza kuitazama Arsenal ikicheza moja kwa moja kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE ROBO FAINALI,” Alinur alisema huku akionesha picha akiwa kwenye ndege.

Akizungumza kama shabiki wa Arsenal, Alinur alisema kuwa ana matumaini ya Zaidi ya asilimia 100 kuwa timu yake itafuzu kuingia nusu fainali kwa kuichabanga mwenyeji Bayern Munich.

Pia alisema kuwa ana mpango wa kuialika timu nzima ya Arsenal kuja Kenya ili kuwapa motisha vijana wapenda soka.

“Nina uhakika 101% Arsenal itaiondoa Bayern Munich nje ya UCL. Pia nitawaalika Arsenal nchini Kenya na kuwakaribisha timu nzima wanapowashauri vijana wetu,” alisema.

Wengi wanahisi kwamba Arsenal ina matumaini finyu ya kufuzu nusu fainali baada ya kuruhusu sare ya 2-2 wiki jana wakiwa nyumbani Emirates.

Katika mechi hiyo, Bayern walicheza bila hata shabiki mmoja uwanjani kutokana na adhabu ya UEFA kwa mashabiki wao kwa kutupa fataki uwanjani katika mechi ya awali dhidi ya Lazio kufuzu robo fainali.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved