Rihanna azungumzia maisha yake ya awali na majuto

alifichua kuwa alistarehe sana kuvaa pajama na sweatpants baada ya kupata mtoto wake wa pili mwaka jana.

Muhtasari
  • Lakini, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ushirikiano wake wa hivi punde na Puma huko London, alisema kujipamba "kunafanya kitu kwako kama mwanamke".
Rocky awafokea walevi kupigana mbele ya mkewe Rihanna
Rocky awafokea walevi kupigana mbele ya mkewe Rihanna
Image: Instagram

Msanii kutoka Barbado Robyn Rihanna Fenty, almaarufu Rihanna alizungumzia maisha yake ya awali na baadhi ya anachojutia kufanya mahojiano yake na VOGUE.

Mwimbaji aliyegeuka kuwa mjasiriamali alifichua, "Najuta kufichua mwili wangu jinsi nilivyofanya." Akijulikana kwa kuchagua mitindo bila woga na mtindo wa kusukuma mipaka, Rihanna alikiri nyakati za kutoamini alipokuwa akitafakari maisha yake ya zamani.

"Itaonekana kuwa unafiki lakini, nimefanya mengi katika maisha yangu. Nilitoa chuchu zangu nje, nilitoa chupi yangu, lakini sasa hayo ndiyo mambo ambayo nadhani sasa kama mama, na kama msichana aliyebadilika singewahi kufanya,” alieleza, akidokeza mtazamo mpya tangu akuwe mama.

Mama huyo wa watoto wawili, ambaye wakati mmoja alitikisa ulimwengu wa muziki kwa sura yake ya ujasiri na mara nyingi ya uchochezi, sasa anakumbuka maisha yake ya zamani kwa mchanganyiko wa kutamani na kutoamini. "Wakati fulani mimi hutazama nyuma na huwa kama 'Oh Mungu wangu, nilifanya hivyo kweli?! chuchu zangu nje?’…Singefanya hivyo sasa hivi,” Rihanna alikiri.

Mwimbaji huyo pia alifunguka kuhusu mapambano yake na mitindo baada ya kuzaa, akifichua kuwa alistarehe sana kuvaa pajama na sweatpants baada ya kupata mtoto wake wa pili mwaka jana.

"Baada ya kupata watoto, mtindo unakuwa kitu ambacho si ya muhimu zaidi," alisema.

Lakini, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ushirikiano wake wa hivi punde na Puma huko London, alisema kujipamba "kunafanya kitu kwako kama mwanamke".

 

Mshindi wa tuzo nyingi za Grammy ana watoto wawili wa kiume na rapa A$AP Rocky - RZA Athelaston Mayers, aliyezaliwa mwaka wa 2022, na Riot Rose Mayers, aliyezaliwa mwaka wa 2023.

"Nikiwa na ujauzito wa kwanza, ninahisi kama niliweza kuvaa viatu vya juu wakati wote," alisema.

"Lakini basi na ujauzito wa pili, una mtoto mchanga, tumbo, ni msimu wa baridi, una kanzu, begi la mtoto. na unajiuliza kama unaweza valia viatu vya juu...... Hmm, labda sivyo. Ndiyo maana nilipata ubunifu zaidi kidogo na mtindo wangu wa starehe.

"Na kisha nilistarehe sana baada ya kupata mtoto wangu wa pili na nilikuwa nimevaa mavazi, PJs, sweatpants.

"Na sasa ninacheza tena. Sasa ninaburudika na nguo zangu.”