Mulamwah aonyesha mtoto wake na Ruth K, Oyando Jr (+picha)

Mwezi uliopita, Ruth K alifichua kuwa mtoto wao hafanani naye hata kidogo ila anafanana sana na Mulamwah.

Muhtasari

•Mulamwah alichapisha picha iliyomuonyesha akiwa amemshika mwanawe na kutumia nafasi hiyo kueleza upendo wake kwake.  

•Mzazi mwenzake, Ruth K pia alichapisha picha hiyo kwenye ukurasa wake na kuwatambulisha kama "Wavulana wangu!"

Mulamwah na mpenzi wake Ruth K
Image: INSTAGRAM// MULAMWAH

Siku ya Jumatano, mchekeshaji David Oyando almaarufu Mulamwah alionyesha kidogo sura ya mtoto wake wa miezi miwili, Oyando Jnr.

Mchekeshaji huyo ambaye pia ni muuguzi alichapisha picha iliyomuonyesha akiwa amemshika mvulana huyo mdogo na kutumia nafasi hiyo kueleza upendo wake kwake.  

"Company," Mulamwah aliandika kwenye picha aliyochapisha kwenye Instagram na kuambatanisha ujumbe huo na emoji za upendo.

Katika picha aliyochapisha, mchekeshaji huyo hata hivyo alificha sehemu kubwa ya uso wa mwanawe kwa mkono wake, ili asionekane vizuri.

Mzazi mwenzake, Ruth K pia alichapisha picha hiyo kwenye ukurasa wake na kuwatambulisha kama "Wavulana wangu!"

Image: INSTAGRAM// MULAMWAH

Takriban mwezi mmoja uliopita, Ruth K alilalamika kwa utani kuhusu ufanano mkubwa wa mwanawe na mzazi mwenzake, Mulamwah.

Akizungumza kwenye video aliyochapisha kwenye Instagram, mama huyo wa mtoto mmoja alibainisha kuwa mwanawe Oyando Jr hafanani naye.

Alidokeza kwamba hata vidole vya miguu na mikono vya mtoto huyo wake wa wiki chache vinafanana na vya Mulamwah.

“Ona mnafanana hadi vidole. Si hanifanani. Wee angalia tu mikono na miguu,” Ruth K alisikika akimwambia mpenzi wake Mulamwah.

Wakati akimjibu mpenzi wake, Mulamwah alimwambia ,” Ongeza bidii”, ushauri ambao Ruth K aliuliza jinsi ungewezekana.

Mulamwah na mpenzi wake Ruth K walitangaza kuzaliwa kwa mtoto wao wa kwanza pamoja mnamo Februari 10, 2024.

Wakati akitangaza habari hiyo njema, Mulamwah alieleza dhamira yake kubwa katika kujenga kumbukumbu na mwanawe.

“MUNGU NI MKUU , hatimaye kijana wetu yuko hapa , mrithi yuko hapa , MFALME yuko hapa - @oyando_jnr aka kalamwah, karibu duniani mwanangu, ni hisia nzuri zaidi ulimwenguni hatimaye kukuona na kukushikilia. siwezi kusubiri sisi kukua na kufanya kumbukumbu pamoja, "alisema.

Pia alimtambua mzazi mwenzake Ruth K, na kumshukuru kwa kumpa mtoto wake wa pili na kuwa naye kila wakati.

"Asante sana @atruthk kwa zawadi hii nzuri na ya kushangaza, asante kwa kuwa karibu nami kila wakati," alisema.

Aliongeza, “Ninahisi mzima tena, nahisi kurejeshwa, nina furaha , familia sasa zina furaha dunia nzima ina furaha , ♥️♥️ . Nakutakia maisha marefu na yenye afya tele kijana wangu na kila la kheri ulimwenguni. baraka tele. Karibu KALAMWAH !! maisha marefu oyando.”