logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Maoni kinzani baada ya NaiBoi ku’post Instagram kwa mara ya kwanza tangu Novemba 2023

“Weee kijana wacha kupotea kama matiang'i hivi” Nikolazgutez

image
na Davis Ojiambo

Burudani26 April 2024 - 08:44

Muhtasari


  • • Mashabiki wake waiokuwa wakimsubiri kwa hamu kuu walifurika katika upande wa kutoa maoni wakimuuliza amekuwa wapi huku wengine wakitoa maoni yenye dhana tofauti.
NAIBOI

Mashabiki wa msanii NaiBoi wamemsakama kwa maswali mengi baada ya kuchapisha kwa mara ya kwanza katika ukurasa wake wa Instagram tangu mwaka jana mwezi Novemba.

Naiboi ambaye anasemekana kuwa nchini Marekani amekuwa mkimya na kutoweka kutoka kwenye tasnia ya muziki wa humu nchini kwa Zaidi ya miaka miwili pasi na kusikika kwa kibao chochote kipya kutoka kwake.

Msanii huyo aliwatia wasiwasi mashabiki wake katika siku za hivi karibuni, baada ya mashabiki hao kubaini uwepo wake katika mitandao ya kijamii pia umekuwa finyu.

Naiboi alionekana kwenye Instagram Novemba 5, 2o24, Zaidi ya wiki 24 alipochapisha picha ya Mfalme wa Uingereza na msanii wa kundi la Sauti Sol, Savara wakati kiongozi huyo alipozuru taifa la Kenya.

Tangu hapo, Naiboi alitoweka bila kuchapisha chochote, jambo lililowashinikiza mashabiki wake kuanzisha kampeni ya kutaka kujua aliko.

Hata hivyo, Aprili 25, 2024, Naiboi alichapisha kwa mara ya kwanza katika ukurasa huo picha yake akiwa ameangalia upande mwingine na kuipa karma mgongo.

Mashabiki wake waiokuwa wakimsubiri kwa hamu kuu walifurika katika upande wa kutoa maoni wakimuuliza amekuwa wapi huku wengine wakitoa maoni yenye dhana tofauti.

Haya hapa ni maoni ya baadhi ya mashabiki;

“Tutasondeka hii tabia ya kuenda missing bila apology😂😂” cara njogu.

“Kuja okoa mziki bana” ephrhym.

“Hatimaye amekumbuka password ya IG” Abbas 4pf.

“Umekuwa wapi?” Adianarossmusic.

“Weee kijana wacha kupotea kama matiang'i hivi” Nikolazgutez

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved