Raburu na Nviiri wazungumzia utafiti ulioweka wanaume wa Kenya kuvutia zaidi barani Afrika

Matokeo ya uchunguzi yanaonyesha kuwa wanaume weusi kwa ujumla wanaonekana kuvutia zaidi kuliko wanaume weupe au wa Asia Mashariki.

Muhtasari
  • Msanii mashuhuri nchini Kenya Bien Aime Baraza, alimtania mkewe akisema, "Mtu amwambie Chiki mimi ndiye tuzo".
Willis Raburu na Nviiri the Storyteller
Image: Instagram

Utafiti wa hivi majuzi uliofanywa na Insider Monkey, umewaorodhesha wanaume wa Kenya kama wanaume wanaovutia zaidi barani Afrika.

Nigeria na Ethiopia zilinyakua nafasi ya pili na ya tatu mtawalia. Rwanda, Afrika Kusini, na Angola zinashika nafasi ya nne, ya tano na ya sita mtawalia.

Matokeo ya uchunguzi yanaonyesha kuwa wanaume weusi kwa ujumla wanaonekana kuvutia zaidi kuliko wanaume weupe au wa Asia Mashariki.

Nviiri the Storyteller na Willis Raburu hawakuweza kukosa kutoa maoni yao kuhusu habari hizo. Nviiri aliposti picha ya skrini ya utafiti huo kwenye Instastories zake na nukuu, "Tutatoa taarifa hivi karibuni. TUNAKUBALI TUZO," huku Willis Raburu alipima uzani kwa emoji ya kijanja.

Instastories
Image: Instagram

Msanii mashuhuri nchini Kenya Bien Aime Baraza, alimtania mkewe akisema, "Mtu amwambie Chiki mimi ndiye tuzo".

Angalia baadhi ya maoni mseto kutoka kwa Wanamtandao;

gacha9ua: Grandma wasn’t wrongπŸ₯ΈπŸ™πŸΎ

unruly_t.ycoon: Ndio maana nimekatiwa na mchina juziπŸ˜‚

nedyparezo: Ni juu tukona iPhone πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

i.am_shakilla: Kwani niko kenya ingine? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

finesse_ngara_: Kwani Niko wapi jameniπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ni hii sura yangu

l_a_v_i_e_1::  Who bribed the judges πŸ˜‚πŸ˜‚

barakawandario: Even Kenyans don't believe this

_therealnica: πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Lies

_.boit.vsthewrld: Wameona tu picha za wasanii hawajaingia pale kakamega

princejay_reborn: Wameona riggy gπŸ˜‚