TID aweka rekodi sawa kuhusu maoni aliyotoa kuhusu Arbantone

TID aliongeza kuwa anapaswa kuambiwa mmoja wa wasanii bora wa arbantone ili wafanye kazi pamoja.

Muhtasari
  • Pia aliulizwa kuhusu maoni yake kuhusu muziki wa Amapiano kwa sababu mwanzoni alisema kuwa haupendi.
TID
TID
Image: INSTAGRAM

Mwanamuziki wa Tanzania Khalid Mohamed anayefahamika pia kwa jina la TID (Top in Dar es Salaam) ameweka rekodi sawa kuhusu maoni aliyoyatoa kuhusu wasanii wa arbantone.

Katika mahojiano yake na Kwambox na Chito, TID alifafanua kuwa sio kwamba hapendi arbantone. Alitoa maoni hayo kwa sababu hakujua mengi kuhusu aina mpya ya mziki ambayo ni arbantone.

“Sikuwa najua mengi kuhusu arbantone. Watu walinieleza kuwa wanasample beats za watu na hiyo aina ni ya kizazi kipya ambayo ni nzuri. Lakini hata kama unatumia beats za mtu mwingine si ni lazima umpee kitu kidogo yenye umepata”, TID alieleza.

Aliongeza kuwa anapaswa kuambiwa mmoja wa wasanii bora wa arbantone ili wafanye kazi pamoja.

“Nataka munipee jina ya msanii mmoja wa arbantone tufanye kazi pamoja na yeye. Nitampea ruhusu ya kutumia beats zangu.”

Awali alikuwa amewatishia wasanii wa arbantone kutotumia sauti yake bila ruhusa.

“Nitakufunga polisi mimi, usifanye hiyo kitu, ukichukua wimbo wangu ufanyie huo arbantone yako bila ruhusa yangu, uko kwenye matatizo mdogo wangu na nitakuchukia maisha yangu yote”, TID alisema kwa hasira.

Pia aliulizwa kuhusu maoni yake kuhusu muziki wa Amapiano kwa sababu mwanzoni alisema kuwa haupendi.

“Mimi amapiano siipendi kwa sababu kila mtu anaifanya na kusahau aina yetu kama muziki wa  bongo. Tunakuza muziki wao sana na hiyo inanikera. Tunapaswa kushikamana tu na aina yetu ya muziki na kuupenda", TID alieleza Kwambox na Chito

Pia alisema kwa utani kwamba watu wanaweza kupita mbele ya mahojiano yake sasa. Hana tatizo na hilo hata kidogo.