Katika hali ya kisikitisha na kutamausha, tiktoker anayeishi Ujerumani, Nyako Pilot amejitabiria kifo chake huku akiwaeleza mashabiki wake ugonjwa ambao amekuwa akiugua kwa muda.
Kupitia kipindi cha mubashara kwenye TikTok, Nyako ambayo mara nyingi huonekana akinywa maji mara kwa mara kweney vpindi hivyo, alifichua kwamba amekuwa akipambana na tatizo la moyo.
TikToker huyo maarufu alifichua kwamba tatizo lake limefikia hatua za mwisho kabisa huku akisema kwamba haoni akiishi Zaidi ya miaka mitatu ijayo.
“Mimi niliwaambia, yale maisha ambayo nimebaki nayo kwa hii dunia nyongeza tu. Mimi ni mgonjwa sana. Kama nitaanza kuwaeleza jinsi afya ya mwili wangu inanifeli siku baada ya nyingine hamwezi amini. Lakini mjue mimi niko katika hatua za mwisho kabisa za ugonjwa wangu, zenye nikisalimika kwa miaka 3 ijayo utakuwa kama muujiza kwangu,” Nyako alianza.
“Kama sitakuwa nimekufa katika kipindi cha miaka 3 ijayo, nitakuwa muujiza unaoishi. Lakini mwisho wa kwisha, sisi wote kwa wakati Fulani tutakufa, uwe mgonjwa usiwe mgonjwa, kifo lazima kitatembelea kila mtu. Mimi kile ninawaomba kuwa makini sana jinsi unavyowafanyia watu, usiwaumize watu,” Nyako alishauri baina ya sauti nzito yenye huzuni.
TikToker iliwashauri zaidi watu kuishi maisha yao na wasisubiri hadi siku watakapolala kwenye vitanda vyao vya wagonjwa na wamejaa majuto
Nyako alisema kwamba yeye amebadilika na kuamua kuwa mtu mzuri, akisema kuwa hatodhalilisha mtu yeyote.
“Na mimi sitaeneza chuki, sina chochote cha kupata nikieneza chuki. Bado nitawaweka pamoja watu kueneza chuki, lakini hiyo sio njia ninayoona mambo. Unaweza ukawa mtu mbaya, na pia unaweza ukawa mtu mzuri, kama unataka kuwa. Kwa hiyo mimi nimeamua kuwa mtu mzuri. Na ugonjwa wangu kwa kweli unaninyenyekesha sana, hili tatizo langu la moyo linaninyenyekesha sana,” Nyako alisema.
Tazama video hiyo yenye hisia kali hapa;