logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Afrikaan Shabba: Chingiboy amshika mkono msanii mwingine baada ya mzozo na Simple Boy

Said Omar Mwacheo, kwa jina la Sanaa Afrikaan Shabba ni mzaliwa wa kaunti ya Mombasa

image
na Davis Ojiambo

Burudani28 April 2024 - 06:01

Muhtasari


  • • Baada ya wiki kadhaa za sekeseke baina yake na Stevo Simple Boy, Chingiboy ameonekana kutoyumbishwa na hilo na sasa ameonesha nia yake ya dhati kumshika mkono msanii mwingine kwa jina Afrikaan Shabba.
  • •  Hata hivyo, Chingiboy anasema kwamba ataendelea kuwashika mkono wasanii wanaohitaji sapoti kwenye tasnia ya muziki inayokwenda kazi.
Afrikaan Shabba, msanii wa dancehall kutoka Mombasa

Aliyekuwa meneja wa msanii Stevo Simple Boy, Chingiboy Mstado ameweka wazi mpango wake wa kuendelea kuwashika mkono wasani wengine haswa chipukizi katika Sanaa ya muziki licha ya kukatishwa tamaa na rapa huyo wa ‘Freshi Barida’.

Itakumbukwa Chingiboy na Stevo katika wiki chache zilizopita walikuwa katika mzozo mkali, meneja huyo akisema familia ya Stevo ilitaka umiliki wa akaunti zake za mitandaoni na kwa upande wake akishikilia kuwa alitaka alipwe kwanza.

Hata hivyo baada ya yote hayo, Chingiboy ameonekana kutoyumbishwa na hilo na sasa ameonesha nia yake ya dhati kumshika mkono msanii mwingine kwa jina Afrikaan Shabba.

Kwa wapenzi wa muziki wa dancehall kutoka upande wa Pwani ya Kenya, Afrikaan Shabba si mgeni wala chipukizi katka muziki, lakini kwa wengi kutoka pande zingine za Kenya, huenda ni mara ya kwanza kwao kusikia jina hili.

 Na hii ndio sababu Chingiboy ameamua kumshika mkono ili kuieneza brand yake kwa mashabiki wa muziki wa Reggae dancehall kutoka pande zingine, kama tu alivyofanya kwa msanii Stevo Simple Boy kabla ya kuota mbawa na kuruka mawinguni.

Said Omar Mwacheo, kwa jina la Sanaa Afrikaan Shabba ni mzaliwa wa kaunti ya Mombasa ambaye amekuwa akifanya muziki wa Reggae Dancehall kwa muda.

Afrikaan Shabba ni mtumbuizaji wa kweli ambaye anajua jinsi ya kuacha hisia ya kudumu kwa Mashabiki wake, kama inavyodhihirika katika baadhi ya kazi zake kwenye chaneli yake ya YouTube.

Kwa uwepo wake wa ajabu wa hatua na talanta isiyoweza kuepukika, yeye hujitahidi kuamuru usikivu wa hadhira yake. Kutokana na kutikisa kwenye bendi wakati wa shule ya upili na matukio ya chuo kikuu kwa kutumia zawadi yake kusaidia shughuli za hisani, utumbuizaji wake huacha alama ya kudumu kwenye vichwa vya hadhira yake.

Katika safari yake ya muziki na azma ya kupenda midundo hiyo yenye asili ya Jamaika, Shabba ameshirikiana na wasani akiwemo Kelechi Africana, Arrow Bwoy miongoni mwa wengine na hata kupata nafasi ya nyimbo zake kuchezwa kweney vituo mbalimbali vya habari, lakini bado amemfuata Chingiboy kwa msaada Zaidi.

Hata hivyo, Chingiboy anasema kwamba ataendelea kuwashika mkono wasanii wanaohitaji sapoti kwenye tasnia ya muziki inayokwenda kazi.

Kando na hio, Chingiboy ameweka wazi kwamba hajafa moyo kuwa meneja wa msanii mwingine, akieleza mpango wake wa kumtambulisha msani mwingine mpya kuchukua nafasi ya Stevo Simple Boy hivi karibuni.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved