Rachel Otuoma, mke wa aliyekuwa mchezaji wa AFC Leopards na Ulinzi Stars, Ezekiel Otuoma amefichua kwamba tangu mume wake agonjeke miaka 4 iliyopita, wamekaa miaka 2 bila kufanya mapenzi katika ndoa yao.
Otuoma ambaye alikuwa katika shoo ya Obinna kwenye YouTube pamoja na mume wake ambaye sasa anatembea kwa kutumia kiti cha magurudumu, alisema kwamba katika kipindi chote cha ugonjwa wa mumewe, amekuwa mwaminifu kwenye ndoa.
Mchezaji huyo mwenye kipawa aligunduliwa na ugonjwa wa motor neurone ambao ulimlemaza baadhi ya viungo vya mwili wake kiasi kwamba hawezi kutembea wala kuzungumza.
Katika shoo hiyo ambayo wanandoa hao walikwenda na kuzungumzia jinsi ugonjwa huo ulivyompata alipokuwa bado anacheza na athari ambayo imekuwa nayo katika maisha yao ya kila siku na yeye kuwa pale kwa ajili yake kwa bora na mbaya Zaidi mkewe alisema kuwa amekuwa akiteseka bila tendo la ndoa kwa miaka miwili.
“Kutoka Otuoma agonjeke, bila shaka ni miaka minne. Tumekuwa katika hii safari kwa miaka 4 na hii hali ikianza, Otuoma alikuwa anatembea. Naweza nikasema kwamba imekuwa ni miaka miwili nimekuwa nikiteseka bila mapenzi. Na kusema ukweli mimi sijawai ‘chukua sheria mkononi’,” Rachel alisema.
Hata hivyo, Rachel alisema kuwa baadhi ya marafiki wa mumewe wamekuwa wakichukulia kama fursa ya Otuoma kuwa mgonjwa na kutaka kumtongoza.
“Kuna wanaume wengi wanakuja DM sikatai. Kwanza mmoja ni rafiki yake [Otuoma], aliona hata ujumbe. Nilimuonyesha nikamuuliza hawa ni marafiki wa aina gani uko nao. Aliniambia eti angependa kunipeleka dinner. Hapana,” alisema.