Mwanamuziki na mtunzi wa nyimbo aliyeshinda tuzo Nikita Kering anasherehekea miaka 10 tangu ajiunge na kuanza kutumia mtandao wa picha, Instagram.
Mkali huyo wa nyimbo za R&b, Afro-Pop na Pop alichukua kwenye ukurasa wake Instagram kufichua hilo na kusherehekea kwa video akiwa anashirikiana na watu kutoka kampuni mama ya Instagram, Meta.
“Kuadhimisha mwaka wangu wa 10 kwenye Instagram kwa ushirikiano na Meta,” Nikita Kering aliandika.
Mashabiki wake waliungana naye kusherehekea wengine wakimpongeza kwa hatua hiyo.
Katika kipindi cha miaka 10, Kering amefanikisha kupata wafuasi Zaidi ya 569k.
Kufichua kuwa amekuwa Instagram kwa miaka 10, na upande mwingine ikijulikana kuwa ana umri wa miaka 22 sasa, kuliibua maswali kutoka kwa wengine ambao walimuuliza kwa utani kama alianza kutumia Instagram akiwa na miaka 12.
“Kwani uliingia Instagram ukiwa 12yrs😅” ian.
“Mungu akisema ndiyo hakuna awezaye kusema hapana😍❤️” signalstephen.
“Hizii deals zakoo unatoanga wapi na hayuko signed ka netflix gig ya bbc na kuna waimbaji wamekaa 20 years na wakoo tu uku kenya sii uwavutishe rada” cachi asani alimwambia.
“Mpendwa Nikita😘 imenibidi kuacha kuperuzi na kuchukua muda wa kupongeza kwa hili. Unaonekana mrembo kabisa! Kuamka kwa tabasamu lako ndiyo njia bora ya kuanza siku yangu. Ninakupenda zaidi ya maneno yanavyoweza kueleza na siwezi kungoja kukuona siku moja. Uwe na siku njema, mi amor,” Shengtezo alimwandikia.
“Hii ndio sababu wewe ni crushiiii” black gramma.