Christina Shusho aeleza sababu yake ya kuolewa akiwa na miaka 19

Hitmaker huyo wa "Shusha Nyavu" alizungumza kuhusu wasiwasi wa mama yake kutokana na urembo wake wa kuvutia, ambao ulimfanya kukimbilia kuolewa.

Muhtasari
  • Katika mahojiano, msanii huyo mashuhuri alihusisha matendo yake na kujitolea kwake kwa wito wake wa huduma.
Shusho amchochea Stevo kuokoka
Shusho amchochea Stevo kuokoka
Image: insta

Msanii wa nyimbo za Injili raia wa Tanzania Christina Shusho ameeleza sababu za kuolewa akiwa na umri wa miaka 19.

Msanii huyo maarufu kwa wimbo "Shusha Nyavu" alizungumza kuhusu wasiwasi wa mamake kutokana na urembo wake wa kuvutia, ambao ulimfanya kukimbilia kuolewa.

Alikuwa amemaliza elimu yake ya kidato cha nne.

“Niliolewa nikiwa na umri wa miaka 19, mchanga sana. Baada ya kumaliza kidato cha nne . Nilikuwa mrembo wa kipekee, na mama yangu aliogopa kwamba ningeweza kupotoshwa na kuleta aibu kwa familia,” Shusho alieleza.

Shusho alitaja kuwa alikuwa mrembo zaidi kitambo sio kama sasa.

“Sasa, mimi ni mkubwa zaidi, usiniambie mimi ni mrembo; Nilikuwa mrembo ajabu. Kwa hiyo, mwanamume huyu alipomwendea mama yangu akionyesha kupendezwa nami, alikubali tu kwa woga. Hakika nilikuwa mrembo sana.”

Katika mahojiano mengine, Christina Shusho alizungumzia uamuzi wake wa kuvua pete ya ndoa na kutengana na mumewe mchungaji, John Shusho.

Katika mahojiano, msanii huyo mashuhuri alihusisha matendo yake na kujitolea kwake kwa wito wake wa huduma.

Alifichua kwamba alikuwa na maono ambayo alikuwa ameazimia kutimiza, na kusababisha kuvunjika kwa ndoa yake kwa amani.

"Siku zote nimekuwa halisii na mkweli. Ukweli ni kwamba ni utume tu. Hakuna kingine kilichobadilika. Kazi ambayo Mungu alinipa wakati huu ilinihitaji niondoke pale nilipokuwa. Ilinibidi kuondoka ili kutimiza misheni,” alifichua kwa uwazi.

Shusho pia alifafanua kuwa hana cheo cha mchungaji na alionyesha kutofurahishwa na kupachikwa jina hilo.