Tiktoker mwenye ulemavu Kennedy Rioba maarufu kama Babushka Kenya amethibitisha kuibiwa simu yake ya iPhone 11.
Kupitia Instagram yake, Babushka alisema kuwa alikuwa katika harakati ya kuabiri matatu wakati mwizi asiyejulikana alimvizia na kumpora simu yake kutoka mfukoni.
Hata hivyo, kijana huyo alisema kwamba amemsamehe mwenye alimfanyia hivyo.
“Siku ndefu kwangu, wakati najaribu kuabiri matatu nikirudi nyumbani, mtu Fulani aliamua kunipora simu yangu, iPhone 11, na ambaye alifanya hivyo nimekusamehe kutoka moyoni,” Babushka alisema.
Kijana huyo aliomba msaada wa simu yoyote ya kutumia wakati anajikusanya kujinunulia nyingine huku akitoa namba yake ya kupatikana kwa ajili ya msaada huo.
“Niko katika hali ya uchungu mwingi kupoteza content nyingi ambayo nilikuwa nimeweka katika simu ile. Yeyote ambaye ako tayari kunisaidia amba yeyote mwenye simu mbili, tafadhali nisaidie na moja. Simu ya aina yoyote tu nitashukuru kutoka kwa wahisani,” Babushka alisema.
Hata hivyo, baadhi ya watumizi wa mtandao wa Instagram walihisi anawachezea shere wakitaka kujua ni simu gani alitumia kuchapisha ujumbe huo wa kuomba msaada wakati anasema ameibiwa.
Hata hivyo, kuna wengine walimhurumia na kushangaa jinsi mwizi aliinama hadi kuiba dimu, kwani TikTok huyo ni mlemavu asiye na miguu.
“Just curious 🤔,,huyo mtu ali inama ama.” Reine 2003p.
“Si kwa ubaya but ume post na nini??” Benorigyn.
“Si huyu ndo niliona alitumia mtu juzi 200 akabaki na balance ya 110k ..kwani amekula yooote😮😮” lameckisaac.
“Huku nje mnapiga ata magoti ndio mwibe😢” james12mawira.