Mtayarishaji wa Maudhui, Flaqo Raz amefunguka kuhusu ni kwa nini mara nyingi huwa haonekani kuwa na ndevu, licha ya kwamba ndevu zake zinaota kila uchao.
Katika klipu moja ya video ambayo alifanya kwenye Instagram yake kuelezea huli, Flaqo alisema kwamba si kweli kuwa haoti ndevu lakini akafichua kwamba yeye hunyoa ndevu zake kila asubuhi anaporauka.
Mkuza maudhui huyo alisema kwamba ameifanya kama ibada kunyoa ndevu zake kila asubuhi, ili kuendeleza maudhui yake ya kuigiza kama mwanamke – Mama Otis na Akoth, akisema kwamba wahusika hao katika video zake za ucheshi ni wanawake na hivyo ili kuwa kama wao, anastahili muda wote kuhakikisha hana ndevu.
"Lazima niamke kila siku na kunyoa. Ni sehemu ya utaratibu wangu. Mama Otis na Akoth hawana ndevu. Ikiwa ningeshika ndevu zangu wahusika hawa wangebadilika. Kwa hivyo hiyo ni nadharia ninayopaswa kufanya kwa kunyoa ndevu zangu, " alisema.
Kijana huyo alisema kwamba alilazimika kufanya video hiyo ya kuelezea kinagaubaga kuhusu ndevu zake baada ya kuona kile alichokitaja kuwa dharau kutoka kwa baadhi ya vijana wadogo ambao walimuona kama mdogo wao na kutaka kumshauri kisa hana ndevu.
Flaqo alisema kwamba alibaki katika hali ya mshangao baada ya kuona kijana huyo wa miaka 20 mwenye ndevu nyingi akimketisha chini na kujaribu kumpa ushauri kuhusu maisha.
Alisema kwamba mpaka wakati anaandaa video hiyo, bado alikuwa katika hali ya mshangao, kisa kushauriwa na kijana mdogo ambaye alimuona kuwa mdogo wake kwa kutokuwa na ndevu.