Baada ya kupashwa na Zuchu, Harmonize ameonekana kubadili fikira zake na kutaka kujaribu bahati yake katika mchezo wa ngumi.
Kupitia insta story yake, Harmonize alisema kuwa amejikita katika mazoezi ili kupambana mchezo wa ngumi na bondia Hassan Mwakinyo, akisema kuwa tasnia ya muziki ina chuki nyingi sana.
“Acha nizingatie katika kumchapa ngumi Mwakinyo ili nibadilishe taaluma. Chuki ni nyingi sana huku [kwenye muziki]. Pengine kutakuwa na amani, najua nitafaulu, Mungu nisaidie,” Harmonize alisema.
Harmonize alisema haya siku moja baada ya kupapurana mitandaoni na Zuchu kisa ubabe wa muziki kwenye takwimu za kutiririsha miziki.
Zuchu alimkalisha chini Harmonize kwa kumtolea takwimu zilizoonyesha kwamba amemzidi kitakwimu, jambo ambalo lilimfanya Harmonize kudai kwamba muziki una chuki nyingi pengine ajaribu kutafuta tulizo la nafsi na Amani kwenye ngumi.
Itakumbukwa wiki chache zilizopita, Harmonize na Mwakinyo walipapurana kwenye chumba la mazoezi.
Wawili hao ambao wamekuwa wakitambiana kwa muda sasa walikaribia kuzichapa kama si uwepo wa baadhi ya wasaidizi wao ambao waliwatenganisha.