Shakib Cham Lutaaya alionyesha uhusiano wake mzuri na watoto wake wa kambo alipokuwa akimsherehekea mtoto wa Zari Hassan, Quincy Tale mnamo siku yake ya kuzaliwa.
Mfanyibiashara huyo wa Uganda mwenye umri wa miaka 32 alikuwa miongoni mwa mamia ya wanamtandao waliomtakia Quincy siku njema ya kuzaliwa chini ya chapisho la Zari kwenye Instagram.
Mwanasosholaiti Zari alichapisha video ya kuvutia iliyomuonyesha akiongea na mwanawe na chini ya video hiyo alimsherehekea kijana huyo alipofikisha miaka 18.
“Heri ya siku ya kuzaliwa Q, siamini tulikuwa tunakuita lil Q. Angalia wewe. Mungu akubariki kwa ajili yangu,” Zari alimwandikia mwanawe chini ya video hiyo.
Mamia ya watumiaji wa mtandao wa Instagram walimiminika chini ya posti hiyo kumsaidia mwanasosholaiti huyo wa Uganda kumsherehekea mwanawe.
Shakib alimtakia heri ya kuzaliwa kijana huyo na kumtambua kama mwanawe.
“Heri ya kuzaliwa mwanangu @quincy.tlale,” Shakib aliandika.
Hii si mara ya kwanza kwa mume huyo wa Zari mwenye umri wa miaka 32 kuonyesha uhusiano wake mzuri na watoto wa mzazi mwenza huyo wa Diamond Platnumz. Katika siku za nyuma amewahi kuonekana akishiriki muda mzuri na watoto wake wa kambo watano na hata kucheza na Tiffah Dangote na Prince Nillan.
Katika video ambayo Zari alichapisha akimsherehekea mwanawe Quincy, alionekana akishiriki mazungumzo nyeti kuhusu mahusiano na mtoto huyo wake wa tatu pamoja na mwanawe wa pili, Raphael Ssemwanga.
Mama huyo wa watoto watano alisikika akiwashinikiza wanawe wachumbiane na wasichana wengi wanavyotaka.
Zari alianza mazungumzo baada ya mtoto wake Raphael kumjulisha kwamba alikuwa akienda kukutana na marafiki zake.
"Niambie ukweli, utakutana na wasichana, sindio? Unajua tunaweza kuongea kuhusu haya mambo..” Zari alimwambia mwanae Quincy.
Quincy hata hivyo alikana kuwahi kuwa na mpango wa kukutana na wasichana, jambo ambalo lilionekana kumshtua sana mama yake.
Mwanasosholaiti huyo alitumia fursa hiyo kumshauri mwanawe kuchumbiana na wasichana, na kumuonya dhidi ya kuchumbiana na wanaume wenzake.
"Napenda kukusikia ukisema utakula na wasichana, kuliko marafiki. Unajua kizazi hiki kimeharibika, tunataka kukuona ukitoka na wasichana. Sijali nyinyi watu kuchumbiana na wasichana,” Zari alimwambia mwanawe.
Mwanawe mwingine, Raphael alifichua kwamba Quincy alikuwa akienda kukutana na wasichana, jambo ambalo lilionekana kuleta utulivu kwa mwanasosholaiti huyo.
“Nimefurahi, nenda ukawaone wasichana. Ni nzuri. Ninawapenda nyinyi watu kwa hilo, kwa sababu jambo linalofuata, nitashtuka nikigundua mtu anachumbiana na mvulana mwenzake. Nenda ukawaone wasichana, wengi kadiri unavyotaka. Nina furaha kuhusu hilo. Niko sawa nayo,” alisema.
Mama huyo wa watoto watano hata hivyo aliwapa wanawe sifa maalum ambazo anataka rafiki zao kike wawe nazo.
"Hakikisha wanapendeza kama mimi, watazeeka kama mimi, warembo kama mimi, wenye akili kama mimi, wachapa kazi kama mimi," aliwaambia wanawe kabla ya kukatishwa na bintiye Tiffah Dangote.
Huku akimgeukia mwanawe mwingine Raphael, mzazi-mwenza huyo wa staa wa bongo Diamond Platnumz alikosoa mtindo wake wa mavazi akisema anaonekana shoga. Alimfanya abadilishe nguo zake kabla ya kuondoka kwenda kuonana na wasichana.