logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Akothee akasirika baada ya mama wa watoto 6 aliyempa makazi kuleta ex wake kuishi naye

Akothee alisema kwamba tukio hio limemuumiza sana na kuona kuwa anatumiwa vibaya.

image
na Davis Ojiambo

Burudani06 May 2024 - 10:38

Muhtasari


  • • “Ili kuzidisha hali hiyo, anamwalika mume wake wa zamani kukaa naye, na kusababisha usumbufu zaidi na hata kuwakosea heshima wafanyakazi wangu. " Akothee alisema.
Akothee

Mjasiriamali Esther Akoth maarufu Akothee ameonesha kutofurahishwa kwake na hatua ya mama  mmoja aliyempa msaada wa makazi kuchukua hatua ya kumkaribisha aliyekuwa mume wake kuishi na yeye katika makazi mapya.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Akothee alisema kwamba anahisi kutumiwa vibaya kwani single mama huyo wa watoto 6 alimlilia kuwa mume wale ameharibu makazi yao na kumuomba msaada wa nyumba, ambapo alikwenda mbele na kumleta ex wake kwa hiyo nyumba ya msaada kutoka kwa Akothee.

“Inaonekana nimekuwa shabaha ya unyonyaji. Kwa ukarimu nimetoa makazi na rasilimali kwa mama asiye na mwenzi aliye na watoto sita, nikiwapa nyumba, ardhi kwa ajili ya kilimo, chakula, maji, umeme bila malipo, na elimu kwa watoto wake wote. Hata hivyo, pamoja na jitihada zangu, mwanamke huyu anaonyesha kutowajibika kwa watoto wake,” Akothee alisema.

Mjasiriamali huyo wa Akothee Safaris alifichua kwamba single mama huyo alimwambia mume wake ndiye aliharibu nyumba alimokuwa akiishi na wanawe, na hivyo kumtaka msaada wa makazi mbadala, lakini baadae akamleta tena huyo ex kwa nyumba hiyo ya msaada.

“Uvivu wake unadhihirika kwa vile anapuuza wajibu wake wa mzazi. Isitoshe, vitendo vya mume wake wa zamani, kubomoa makazi yake ya awali, vimemfanya kutafuta hifadhi katika boma langu bila ruhusa. Yeye huingia nyumbani kwangu kwa uhuru na kujisaidia kwa chochote anachotaka bila kujisumbua kuuliza.”

“Ili kuzidisha hali hiyo, anamwalika mume wake wa zamani kukaa naye, na kusababisha usumbufu zaidi na hata kuwakosea heshima wafanyakazi wangu. Hali hii imeniacha kuhoji hekima ya ukarimu wangu wa awali na kujiuliza jinsi nilivyoingia katika hali hiyo yenye matatizo,” alimaliza akisema kwamba tukio hilo limemuumiza sana.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved