logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Wewe ni mtu mzuri na utaenda mbinguni” – Milly Chebby ammwambia mumewe Terence Creative

"Mungu usipofanya jambo lingine umefanya zaidi ya kutosha, nisisahau hilo, nashukuru kwa yote uliyonipa"

image
na Davis Ojiambo

Burudani06 May 2024 - 07:24

Muhtasari


  • • Akionekana kuwa na furaha, Terence Creative alijiandiia ujumbe maalum kwa kuongeza mwaka mwingine mmoja katika mzunguko wa maisha.
TERENCE na Mkewe

Mchekeshaji maarufu wa Kenya, Terence Creative alisherehekea siku yake ya kuzaliwa wikendi iliyopita kwa njia maalum.

Akionekana kuwa na furaha, Terence Creative alijiandiia ujumbe maalum kwa kuongeza mwaka mwingine mmoja katika mzunguko wa maisha.

Mchkeshaji huyo ambaye amepiga marufuku watu dhidi ya kutumia maudhui yake kwenye insta stories zake aliweka wazi kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, ameweza kufanikisha vitu vingi, na ni jambo la kumshukuru Mungu.

“NAMSHUKURU MUNGU KWA MWAKA MWINGINE 🙏🎂🎂Mungu usipofanya jambo lingine umefanya zaidi ya kutosha, nisisahau hilo, nashukuru kwa yote uliyonipa, Asante kwa Neema, rehema na afya kwa kutaja tu lakini machache uliyofanya,” Terence alisema.

“Bwana endelea kunipa hekima ya kuthamini nilichonacho kila wakati nikitafuta nisichonacho, nikumbushe kila wakati kushiriki nilichopata sababu sikuwa nacho hapo awali, naomba usiwahi kuzoea miujiza yako midogo ambayo umefanya hapo awali, sasa na miaka ijayo. Nakushukuru Mungu kwa mwaka huu mpya na nyingi utakazonijalia sawasawa na mapenzi yako, zitumike kulitumikia kusudi lako, kukutukuza siku zote na kuathiri wengine, utukuzwe kila wakati katika hali zote,” alimaliza.

 Kwa upande wake, mkewe Milly Chebby alimsherehekea akimtaja kama mtu mzuri ambaye ataenda mbinguni moja kwa moja.

“Happy Birthday Babe @terencecreative. Wewe ni mtu mzuri na utaenda mbinguni ️ Tuma matakwa ya siku ya kuzaliwa kwa Mwenzi wangu,” Milly Chebby alimwandikia.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved