Rapa Stevo Simple Boy amegonga vichwa vya habari baada ya madai yaliyoelekezwa kwa mpenzi wake wa zamani Pritty Vishy.
Wawili hao walikuwa kwenye uhusiano kwa miaka kadhaa hata kabla ya Stevo kuwa maarufu.
Hata hivyo waliachana mapema 2022 na Stevo tangu alipohama na kuoa mwanamke mwingine. Ripoti hata hivyo zinaonyesha kuwa hayuko tena na mke.
Pritty Vishy kwa upande mwingine hajulikani yuko kwenye uhusiano wowote, ingawa ameacha maoni yake kuwa anachumbiana mara kadhaa.
Hata hivyo, katika mahojiano yake na Kenya Online Media hivi majuzi, Stevo alihojiwa kuhusu jambo moja analolikosa kuhusu ex wake huyo na kusema;
“Hakuna.”
“Ju amenichafulia jina kwa mtandao na sijamjibu kwanza msamaha anafaa atoe 50,000 an akitaka turudiane alete laki tano na akitaka nimpachike mimba alete 1 million. Akitaka tufanye harusi milioni 2,” rapper huyo ambaye hakuwa na mzaha alisema.
Pritty Vishy hata hivyo amejibu matamshi ya Stevo, akisema anapaswa kumwambia ana kwa ana.
"Ndo kuamka naenda kuona msanii huyo aseme hizo maneno anaropokwa aniambie kwa uso, naona ngotoo ikitembea," aliandika.
Hapo awali, Pritty alikiri kwamba yeye ndiye aliamua kumaliza mambo na Stevo.
Mwanasosholaiti huyo pia alisema kuwa hatarudiana tena na Stevo, hata kama atamwomba nafasi nyingine.
Mtunzi huyo wa kibao wa ‘Freshi Barida’ alibainisha kuwa tayari amepanda bei.
Vishy alitengana na Simple Boy mapema mwaka wa 2022, miezi michache tu baada ya mahusiano yao kujulikana hadharani.
Wawili hao hata hivyo ilidaiwa hawakuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi kwani Stevo Simple Boy alidaiwa kutaka kusubiri ndoa kabla ya kushiriki tendo la ndoa na mtumbuizaji huyo mwenye umri wa miaka 21.
Katika mahojiano ya mwaka jana, Stivo alidokeza kwamba alichumbiana na Pritty Vishy wakati bado akiwa na mke wake, Grace Atieno. Alisema alipima tabia za wawili hao kabla ya kuamua mke wa kuwa naye.
"Ukiwa na wasichana wawili unaangalia ni nani ako na utu, na ni nani ako wema na unyenyekevu. Kwangu mimi, unyenyekevu na kuvumilia kwake zilifanya nikavutiwa kwake," alisema msanii huyo kutoka mtaa wa Kibera.