Aliyekuwa mtangazaji wa TV Kimani Mbugua, amezua wasiwasi miongoni mwa baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ustawi wake katika video ya kutatanisha aliyoichapisha kwenye mitandao yake ya kijamii.
Kimani, ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa Bipolar, hivi majuzi alichapisha kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii, akimtaka yeyote anayemdai pesa alipe haraka la sivyo atakabiliwa na makosa.
Katika video hiyo macho yake yanaonekana kuwa mekundu.
Kuchunguza kwa karibu machapisho yake kunaonyesha hali ya kutatanisha inayoonyesha kwamba anaweza kuhitaji usaidizi haraka.
Kuona video hiyo, Oga Obina amejitolea kumsaidia kijana huyo huku akiwataka watu wengine kiumsaidia Kimani.
Katika video kwenye mitandao yake ya kijamii Obinna alinukuu, "Wanaume hebu tumsaidie Kimani Mbugua ajisaidie. Piga DM yangu tumtafute na umpeleke mahali aweze kusaidiwa kitaalamu.”
Obinna alishauri kuwa kushiriki video za Kimani mtandaoni kwa likes hakumsaidii na kupuuza hali hiyo huku ndugu yao akitatizika si nzuri.
“Tutafute hospitali, tumlaze, atatushukuru baadaye,” Obinna aliwaita wanaume wengine wenye mawazo kama hayo ili kuficha uchi wa ndugu yao.
Mchekeshaji huyo pia alifichua kwenye video hiyo kuwa awali alimwalika Kimani kwa mahojiano kwenye kipindi chake lakini hakufika licha ya kutumia nauli.
Obinna hata hivyo alithibitisha kuwa hayo ni maji chini ya daraja na sasa matakwa yake ni kwamba waungane na kumsaidia Kimani kupata matibabu kabla ya hali yake kuwa mbaya.
Mtangazaji huyo wa zamani wa redio pia alikiri kwamba ingawa wanajaribu kumsaidia Kimani, huenda mambo yakaharibika kwa kuzingatia hali yake ya Bipolar lakini angalau wanapaswa kufanya juhudi.
Kufikia sasa wanaume hao mtandaoni wanamuunga mkono licha ya mijadala ya awali kutoka kwa wengi wakidai Kimani anajifanya tu.