logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Dem wa FB atimiza ndoto ya kupandisha babake ndege kwa mara ya kwanza maishani mwake

Alimlipia babake nauli ya Ndege kutoka Nairobi kuelekea Eldoret.

image
na Davis Ojiambo

Burudani09 May 2024 - 07:52

Muhtasari


  • • Dem wa FB alifichua kwamba babake alimtembelea kuja Nairobi na wakati wa kurudi Magharibi mwa Kenya, akamlipia nauli ya ndege kutoka Nairobi kuelekea Eldoret.
Dem wa FB.

Mchekeshaji na mkuza maudhui chipukizi, Dem wa Facebook ameonyesha furaha yake baada ya kufanikiwa kutimiza ndoto ya muda mrefu ya kumlipia nauli ya ndege baba yake.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Dem wa FB alichapisha picha akiwa na babake katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKIA.

Alisema kwamba hii ndio ilikuwa mara yake ya kwanza katika maisha ya babake kusafiri kwa kutumia ndege, kwa hisani yake.

Dem wa FB alifichua kwamba babake alimtembelea kuja Nairobi na wakati wa kurudi Magharibi mwa Kenya, akamlipia nauli ya ndege kutoka Nairobi kuelekea Eldoret.

“Dem Wa Facebook Alimshangaza Babake kwa safari yake ya kwanza ya ndege baada ya kumtembelea Nairobi. Safari hiyo ilikuwa kutoka Nairobi hadi Eldoret. "Safari njema baba nakupenda, sitakukatisha tamaa kamwe" Dem wa FB aliripoti kupitia ukurasa wake.

Aidha, aliwashukuru mashabiki wake pamoja na bosi wake, Oga Obinna ambaye amempa nafasi ya kufanya kazi naye kwenye vipindi vyake vya mtandaoni kupitia chaneli ya YouTube, Obinna Show Live.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved