Rapa King Kaka jina halisi Kennedy Ombima, amejishindia Shilingi milioni 1.2 kutoka kwa dau la kandanda.
Jioni ya Jumatano, Mei 8, mwanamuziki huyo aliweka dau lake kwenye pambano la nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Real Madrid na Bayern Munich. Utabiri wake kwamba Real Madrid wangeibuka washindi ulizaa matunda.
Mabingwa hao wa ligi kuu ya Uhispania waliishinda Bayern Munich kwa mabao 2-1, katika dakika za mwisho za mchezo. Akisherehekea ushindi wake kwenye Instagram, King Kaka , alionyesha picha ya iliyothibitisha ushindi wake wa KSh 1.2 milioni kutoka kwa hisa ya KSh 655,000.