Mchekeshaji huyo alibainisha kuwa alinunua ardhi katika maeneo tatu kupitia sanaa yake na kufichua mipango ya kuoa wake watatu.
Mchekeshaji huyo alieleza kuwa anatoka katika ukoo wa wanaume wenye wake wengi, hivyo anakusudia kuendelea na mtindo huo wa Maisha.
Katika mahojiano, Chipukeezy alifichua kuwa ana mpango wa kustaafu akiwa na miaka 40 na kuongeza kuwa kwa sababu ana ardhi katika sehemu tatu tofauti, kwa hivyo ataoa mabibi zaidi ya mmoja.
“Sina haraka ya kuoa ila nataka kustaafu kabla sijafikisha miaka 40 hivyo kabla sijafikisha miaka 40 nitakuwa nimeshaoa nitastaafu na kuja huku siwezi kuwa na mke mmoja nina kipande cha ardhi hapa, na nina ingine upande huu mwingine, nina nafasi ya wake watatu ambao ninaweza kuwatunza," alisema.
Chipukeezy pia aliomba watu waunge mkono hoja yake ya kuha na wake wengi badala ya kuunga mkono wale wanaotetea ndoa za jinsia moja.
"Kwa nini waunge mkono wanaume mashoga? Badala ya kuunga mkono wale ambao wanataka kuha na mabibi wengi" alisema.
"Hatuwezi kuwa na mjadala huu. Ukiniona sina mtu, ujue tu kwamba kuna walio likizo au wametoka; mimi ni mume wa wake wengi na ninajivunia," aliongeza.