logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Obinna wamchukua Kimani Mbugua, waenda naye Mathare huku wakingoja hatua zaidi

Obinna alifichua kuwa yeye na wenzake walimchukua Kimani kutoka nyumbani kwa ajili ya usaidizi maalum.

image
na Samuel Maina

Burudani16 May 2024 - 12:49

Muhtasari


  • •Obinna ametoa taarifa kuhusiana na aliyekuwa mtangazaji wa runinga Kimani Mbugua ambaye anadaiwa kuwa na matatizo ya kisaikolojia.
  • •Aliambatanisha taarifa yake na video yake na wengine wakimchukua Kimani kutoka Thika.
alimchukua Kimani Mbugua Alhamisi

Mtayarishaji wa maudhui Oga Obinna ametoa taarifa mpya kuhusiana na aliyekuwa mtangazaji wa runinga Kimani Mbugua ambaye anadaiwa kuwa na matatizo ya kisaikolojia.

Katika taarifa yake Alhamisi alasiri, mchekeshaji huyo alifichua kuwa yeye na wenzake walimchukua Kimani kutoka nyumbani kwa ajili ya usaidizi maalum.

Alifichua kuwa walimepita katika Hospitali ya Mathare na walikuwa wakingojea wazazi wa mtangazaji huyo wa zamani wa TV kutoa maagizo ili waendelee.

"Sasisho la haraka.. tulimchukua Kim fomu thika, tukapia Mathare na sasa tunangoja maagizo kutoka kwa Baba na Mama kisha tuendelee," Obinna alisema kupitia taarifa kwenye Instagram.

Aliambatanisha taarifa yake na video yake na wengine wakimchukua Kimani kutoka Thika.

"Tutatoa sasisho la mwisho ifikapo jioni kwenye hitimisho," aliongeza.

Hivi majuzi, babake Kimani Mbugua alishiriki mahojiano na Obinna ambapo alifichua kuwa mwanawe alikuwa katika mazingira salama chini ya uangalizi mkali kutoka kwa wanafamilia waliokuwa wakimfuatilia.

Akigusia masuala ya afya ya akili ya mwanawe, mjasiriamali huyo mkongwe alidokeza kuwa masuala ya Kimani yake yalianza miaka minne iliyopita baada ya kinywaji chake kudaiwa kuwekwa dawa alipokuwa akitoka kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Babake Kimani anashikilia kuwa walikuwa na ushahidi halisi wa madai hayo lakini cha kusikitisha waliupoteza.

"Alikuwa na bash, ilikuwa birthday yake na ilikuwa kubwa. Yule dada alichukua simu yake akapitia picha alikuwa anaanguka akitapika na kuna wasichanna wanampiga.

Binti yangu alisema aliona glasi ya mvinyo ikiwa imeongezwa vitu vyeupe, na aliambiwa anywe, na kusababisha kutapika. Na anaambiwa kunywa na anatapika na anaanguka," babake Kimani aliambia Obinna huku akitaja siku hiyo ya tukio mwaka wa 2020 kuwa chanzo cha matatizo ya mwanawe.

Babake Kimani aliendelea kuongeza kuwa baada ya ripoti ya sumu iliyofanywa, waliarifiwa kwamba mtangazaji huyo wa zamani alikuwa na athari nyingi za bangi katika mfumo wake na vile vile dawa zingine chache.

"Basi nilimwambia binti yangu kama tunaweza kuunganisha simu lakini jinsi ilivyopotea hatujui. Tulitaka ushahidi uliokuwepo. Tulifanya toxicology ikagundulika kuna bangi na vitu vingine, nilifanya uchunguzi wangu. na nikagundua marafiki zake wengi walikuwa kwenye vitu hivyo. Kwa hivyo nilihitimisha kuwa mtoto wangu alikuwa amechanganyikiwa na dawa ngumu," alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved