logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rudeboy ashauri wanaume pia kukataa uhusiano wowote wa kimapenzi na mwanamke fukara!

Rudeboy alisema kwamba wanaume wengi wanapitia aibu zilizokithiri mikononi mwa wanawake .

image
na Davis Ojiambo

Burudani19 May 2024 - 06:13

Muhtasari


  • • Msanii huyo kupitia instastory yake aliwauliza wanawake watajihisi vipi ikiwa wanaume pia wataanza kuchagua wanawake wenye hela.
Rudeboy

Paul Okoye, maarufu kama Rudeboy kutoka kundi la muziki wa Afrobeats la PSquare amezua gumzo mitandaoni baada ya kuwashauri wanaume pia kukumbatia hulka ya kukataa mpenzi wa kike asiye na hela, kama wanavyofanya wanawake wengi.

Ifahamike kwamba idadi kubwa ya wanawake wakati wa kufanya chaguo la mwanamume wa kuingia katika uchumba naye, wengi huangalia kigezo cha ‘mwanamume mwenye hela’ na kama huna hela mtoto wa kiume unakataliwa papo hapo.

Sasa Rudeboy anahisi kwamba ni wakati wanaume pia waanze kufuata mkondo huo, akisema kuwa kama wanawake wanavyochagua mwanamume mwenye hela wakati wao hawana chochote cha kuchangia katika mapenzi, basi pia wanaume waanze kuchagua ‘mwanamke mwenye hela’ na kama hana akwende zake pia.

Msanii huyo kupitia instastory yake aliwauliza wanawake watajihisi vipi ikiwa wanaume pia wataanza kuchagua wanawake wenye hela, je wengi wao watapata wapenzi kweli ama wataishia pia kulia.

Rudeboy alisema kwamba wanaume wengi wanapitia aibu zilizokithiri mikononi mwa wanawake wanapopeleka ombi lao la kutaka mapenzi, wengi huishia kusimangwa na kutukanwa vibaya kisa hawana hela.

“Tafadhali wanaume wenzangu, acheni kuoa wanawake mafukara… kwenu nyinyi wanawake, hiyo inaeleweka aje? Mbona kila wakati mnawaaibisha wanaume kisa ufukara? Nafikiri ni wakati wanaume waanze kuchumbiana na wanawake wenye haiba zao kupitia hali zao za kifedha,” Rudeboy alisema.

Je, unakubaliana na maoni yake?

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved