logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Eric Omondi kutumia mamilioni kwa ‘birthday’ ya kwanza ya bintiye

Hio siku tutatafuta jinsi watu watapewa holiday wasiende kazini. Kwa sababu yeye ni binti mfalme

image
na Davis Ojiambo

Burudani21 May 2024 - 13:40

Muhtasari


  • •Hio siku tutatafuta jinsi watu watapewa holiday wasiende kazini. Kwa sababu yeye ni binti mfalme.
  • •Kama tutahamua kuwahalika watu wote tutaweka pale Nyayo kila mtu akuje amuone

Mchekeshaji Eric Omondi alisema yuko tayari kugharamia karamu kubwa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuzaliwa kwa bintiye.

Wapenzi hao wawili walimkaribisha mtoto wao wa kwanza pamoja mnamo Agosti 9, 2023.

Eric Omondi sasa asema yuko tayari kumpa bintiye siku ya kuzaliwa yenye thamani ya kukumbukwa.

Omondi alisema kuwa angewapa mashabiki wake likizo siku hio ya kuzaliwa ya bintiye.

‘Hio siku tutatafuta jinsi watu watapewa holiday wasiende kazini. Kwa sababu yeye ni binti mfalme. Yeye ni binti wa Mfalme na Malkia. Kutakua na siku ya kuzaliwa moja Kisumu. Kutakua na injini Murang’a na injini Nairobi.”

Eric alisema kuwa kama sherehe hio hitakuwa ya watu wote inawezekana kuwa ataiweka katika uwanja wa Nyayo.

“kama tutahamua kuwahalika watu wote tutaweka pale Nyayo kila mtu akuje amuone” Eric alielezea.

Hivi majuzi Eric alifichua mipango yake ya kuongeza mabinti zaidi na Lynn.

 Eric alifichua kwamba alifurahi zaidi kupata mtoto wake mwenyewe baada ya kungoja kwa subira kwa miaka 41.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved