Maombi maalum ya mtangazaji Gidi kwa binti yake Marie-Rose anapotimiza miaka 8

Msichana huyo mdogo anayeishi na mama yake nchini Ufaransa anatimiza miaka minane.

Muhtasari

•Gidi ametumia fursa hiyo kumtakia bintiye kheri ya siku ya kuzaliwa na kueleza upendo wake mkubwa kwake.

•Aliambatanisha taarifa hiyo na picha nzuri ya kumbukumbu yake na Marie-Rose wakiwa nchini Ufaransa.

Mtangazaji Gidi na binti yake Marie-Rose
Image: INSTAGRAM// GIDI OGIDI

Binti ya mtangazaji Joseph Ogidi almaarufu Gidi, Marie-Rose Ogidi anasherehekea siku yake ya kuzaliwa hivi leo, Mei 21.

Msichana huyo mdogo mrembo anayeishi na mama yake nchini Ufaransa anatimiza miaka minane.

Gidi ametumia fursa hiyo kumtakia bintiye kheri ya siku ya kuzaliwa na kueleza upendo wake mkubwa kwake. Pia ameomba kwamba msichana huyo mdogo akue kuwa mtiifu na Mcha Mungu Mungu.

"Ni siku ya kuzaliwa ya Marie-Rose, Kheri ya siku ya kuzaliwa NyarKanyamwa. Uzidi kuwa mtiifu na msichana anayemuogopa Mungu. Upendo mwingi ❤️🙏,” Gidi aliandika kwenye Instagram.

Aliambatanisha taarifa hiyo na picha nzuri ya kumbukumbu yake na Marie-Rose wakiwa nchini Ufaransa.

Mwanzoni mwa mwaka uliopita, mtangazaji huyo wa kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi kwenye Radio Jambo alitumia likizo yake kutembelea familia yake nchini Ufaransa na kuwa na wakati mzuri na binti yake mdogo Marie-Rose ambaye bila shaka ana uhusiano wa karibu sana naye.

Gidi na bintiye walitengeneza kumbukumbu nzuri pamoja wakati wa kikao chake cha muda mfupi na alipokuwa akijiandaa kurejea Kenya, kwaheri yao haikuwa rahisi na iligeuka kwa kipindi cha kihisia kama alivyoonyesha mtangazaji huyo kwenye video.

"Kwaheri sio rahisi😫," Gigi aliandika chini ya video fupi aliyochapisha kwenye mtandao wa Instagram akimfahamisha bintiye kuwa anarudi Kenya na kumuaga kwaheri.

Kwenye video hiyo, Marie-Rose alionekana akiwezwa na hisia pindi tu baada ya baba yake kumuarifu kwamba anataka kuondoka ili kurudi nchini Kenya.

"Marie-Rose, narudi Kenya," Gidi anasikika akimwambia bintiye.

Punde baada ya kusema hayo, binti yake alijibu kwa 'Hapanaa' kubwa na kuweka sura ya uso inayoonyesha kwamba hakutaka aondoke.

Mtangazaji huyo alipomuuliza bintiye ujumbe wa mwisho kwake kabla ya kuondoka, Marie-Rose alijibu, "Nitakumiss."

Pia alimhakikishia malkia huyo mdogo kwamba angemkosa sana pia baada ya kuondoka. Wawili hao kisha walionekana wakikumbatiana kihisia.