logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Amarah: Fahamu maana na chimbuko la jina la mtoto wa Marioo na Paula Kajala

Baadhi ya lakabu za Amarah ni pamoja na Ami, Mara, Arah, Rami, na Hama

image
na Davis Ojiambo

Burudani23 May 2024 - 08:24

Muhtasari


  • • Ingawa mzizi wa neno Amarah ni lahaja iliyoenea ya Amara, vibadala vingine vya karibu vyenye etimologia tofauti vinaweza kujumuisha Amura, Amare, Amer, Amaro, na Ameerah.
  • • Baadhi ya lakabu za Amarah ni pamoja na Ami, Mara, Arah, Rami, na Hama.
  • • Amarah limepata umaarufu mkubwa katika karne ya 21, na kufikia kilele chake mnamo 2019 kukiwa na watoto 206 kwa milioni nchini Marekani wanaoitwa Amarah.
Marioo na mpenziwe Paula.

Katika miaka ya nyuma, watoto haswa katika jamii nyingi za Kiafrika walikuwa wanapatiwa majina ya Kiafrika kuambatana na mila, desturi na miiko ya jamii husika.

Wengi walikuwa wanapatiwa majina kuambatana na nyakati za kuzaliwa, tukio lililojiri wakati wa kuzaliwa, misimu na wengine kupewa majina baada ya watu tajika na wenye ushawishi katika jamii ambao wameshatangulia mbele za haki.

Lakini desturi hizo zinaonekana kumomonyoka kwa kasi katika kizazi cha sasa ambao wengi wameonekana kuyatenga majina ya kiukoo na kijamii na kukumbatia majina mazuri yenye maana tofauti tofauti kutoka mataifa ya ughaibuni, haswa mataifa ya Magharibi na Ulaya.

Katika maboma mengi kwenye jamii za Kiafrika, haswa humu nchini Kenya, utapata watoto wa kizazi cha sasa wakiitwa majina kama Jaydem, Liam, Kai, Amelia, Layla, Olivia, Kyla, Emma, Amaya, Amarah, miongoni mwa majina mengine ambayo huwezi kupata maana ya moja kwa moja, kama ilivyokuwa katika mfumo kwa kupeanwa kwa majina ya watoto zamani.

Moja kati ya wazazi wapya ambao wamekwenda kwenye mkondo huo ni msanii wa Bongo Fleva Marioo na mpenzi wake Paula, ambao wamebarikiwa na mtoto wao wa kwanza mapema wiki hii.

Wazazi hao wapya kabisa hawakusita kuweka wazi jinsia na jina la mwanao, wakimuita Princess Amarah.

Katika Makala haya, tunaangazia Zaidi maana ya jina ‘Amarah’ lakini pia chimbuko lake.

Kwa mujibu wa Mom Junction, Amarah ni jina la kisasa la kike lenye mizizi ya Kiafrika-Amerika, linajitokeza kama kibadala cha kipekee cha Amara.

Katika jamii ya Igbo kutoka Magharibi wa Afrika, jina Amarah linaashiria 'neema,' Huku katika Kisanskrit, moja ya jamii kubwa ya Wahindi, linawakilisha 'asiye kufa' au 'wa milele.'

Asili yake ya Kiarabu inarejelea 'kundi kubwa la meli zinazosafiri pamoja' au 'kabila la kushangaza, Amarah pia jina la mji wa kusini-mashariki mwa Iraqi, na kuongeza utofauti wake.

Ingawa mzizi wa neno Amarah ni lahaja iliyoenea ya Amara, vibadala vingine vya karibu vyenye etimologia tofauti vinaweza kujumuisha Amura, Amare, Amer, Amaro, na Ameerah.

Baadhi ya lakabu za Amarah ni pamoja na Ami, Mara, Arah, Rami, na Hama.

Amarah limepata umaarufu mkubwa katika karne ya 21, na kufikia kilele chake mnamo 2019 kukiwa na watoto 206 kwa milioni nchini Marekani wanaoitwa Amarah.

Ingawa kulikuwa na upungufu kidogo mnamo 2022, na watoto 150 kwa kila milioni walio na jina hilo, bado ni chaguo maarufu na msokoto wa kisasa wa tahajia.

Kwa hivyo, jina hilo linaweza kuvutia wazazi wakitafuta jina la kihistoria na la kupendeza kwa mtoto wao.

Kwa asili na maana zake mbalimbali za neema, kutokufa, na kutokuwa na kabila, inashikilia mvuto na umuhimu wa kushangaza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved