Mbunge wa Mumias East Peter Salasya kwa mara nyingine ameangaziwa sana na wanamitandao kutokana na video yake ya mtandaoni iliyosambaa kwenye X (Twitter).
Katika video hiyo, Salasya anaonekana akifurahia kinywaji chake mezani, huku akizungumzia maswala ya uchumi ya humu nchini. Anatatizika kuzungumza anapotoa maoni yake kuhusu Mswada wa Fedha.
Salasya anaendelea kuelimisha Ruto kuhusu Mswada wa Fedha huku akitaka rahisi Ruto kuinga mfano wa kiongozi wa Marekani anayempenda sana.
“Lazima ajifunze kutoka kwa rais mmoja ninayempenda sana Ronny Reagan. Aliwahi kuwa gavana na akapata uchumi ambao ulikuwa mgumu. Alianzisha kile alichokiita Reaganomics, ambapo aliifanya Amerika kuhama kutoka uchumi wa kati hadi uchumi wa daraja la kwanza," alisema.
Aliendelea kumshauri Ruto apunguze ushuru ambao Wakenya wanalipa, huku akisema pia anampenda raisi Ruto.
“Lazima akubali jambo moja; kupunguza kodi na bajeti ili kuvutia uwekezaji katika nchi hii. Mimi binafsi nampenda rais lakini lazima ajiangalie. Na tutengeneze nafasi za kazi hapa kwetu na kutafuta wafadhili ambao watawekeza hapa nchini na huwezi kuua ndege wawili kwa jiwe moja utafeli sana.” Alieleza.
Video ya Salasya imezua hisia tofauti kutoka kwa Wakenya kwenye X, huku wengi wao wakimwita kwa kuwa mlevi siku ya wiki.